Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Tabia Itakayotambuliwa na Ulimwengu, Sura ya 105

    Mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaoonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu. Wafilipi 2:15.Mar 113.1

    Mungu anakusudia kudhihirisha kanuni za ufalme wake kupitia kwa watu wake. Anakusudia kuwatenganisha na mila, mazoea, na vitendo vya kidunia ili katika maisha yao na tabia zao wafunue kanuni zake... Tabia ya Mungu itakuwa imewasilishwa katika ulimwengu pale ambapo ulimwengu utakuwa umeona wema, rehema, haki na upendo wa Mungu katika kanisa lake. Wakati sheria ya Mungu itakapokuwa imeelelezwa hivyo katika maisha, ulimwengu pia utatambua ya kwamba wale wampendao, wamchao na kumtimikia Mungu ni bora kuliko watu wengine wote.Mar 113.2

    Waadventista wa Sabato, wanapaswa kuwa kielelezo kuliko watu wengine wote katika utauwa, kuwa watakatifu mioyoni na kwenye mazungumzo yao. Hawa wamekabidhiwa kweli zilizo takatifu ambazo mwanadamu amewahi kupewa. Kila kipaji cha neema na uwezo na ufanisi kimetolewa kwa ukarimu mkubwa. Hawa wanadumu katika kutazamia marejeo ya Kristo katika mawingu ya mbinguni jambo ambalo limekaribia sana. Kwa hawa, kutokuweka mwonekano kwamba imani yao ni nguvu inayoweza kutawala katika maisha kunamdhalilisha Mungu kwa kiasi kikubwa.Mar 113.3

    Kwa sababu ya kuongezeka kwa nguvu ya majaribu ya Shetani, nyakati tunazoishi ni za hatari zaidi kwa watoto wa Mungu, na hivyo tunahitaji kujifunza kwa Mwalimu Mkuu bila kukoma, ili tuweze kuchukua kila hatua kwa uhakika na katika haki. Matukio ya ajabu yanafunguka mbele yetu; na katika wakati kama huu ushuhuda hai unapaswa kubebwa maishani mwa watu wajiitao kuwa ni wa Mungu, ili ulimwengu upate kuliona hilo katika kizazi hiki, wakati uovu unapotawala kila upande, bado wapo watu wanaoweka pembeni nia zao na kutafuta kutenda mapenzi ya Mungu -watu ambao ndani ya mioyo yao sheria ya Mungu imeandikwa...Mar 113.4

    Mawazo ya hawa ni safi, maneno yao ni adili na yanayojenga. Dini ya Kristo inapaswa kufungamana kikamilifu na yote wayatendayo na kuyasema. Wanapaswa kutakaswa, kusafishwa, kuwa watu watakatifu, wakiwasiliana na wengine wote wanaokutana nao kuhusu ile nuru. Makusudi ya Mungu ni kwamba wanapokuwa wakieleleza kweli katika maisha yao, watakuwa sehemu ya sifa katika dunia. Ili hili litokee, neema ya Kristo inatosha.Mar 113.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents