Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kwa Nini Kristo Anachelewesha Ujio Wake, Sura ya 53

    Lakini, ndugu, nasema hivi, muda ubakio si mwingi... 1 Wakorintho 7:29Mar 61.1

    Katika ujumbe wao kwa wanadamu, malaika wa Mungu wanawa- silisha muda kama ulio mfupi sana. Ilivyo ndivyo ambavyo umewasilishwa kwangu. Ni kweli ya kwamba muda umekuwa mrefu kuliko tulivyotarajia tulipoanza kuutangaza ujumbe huu. Mwokozi wetu hakutokea kwa haraka kama tulivyotarajia. Lakini je, neno la Bwana limeshindwa? Kamwe! Ikumbukwe ya kwamba ahadi na vitisho vya Mungu pia ni vya masharti.Mar 61.2

    Mungu amewakabidhi watu wake kazi ambayo inapaswa kukamilishwa hapa duniani. Ujumbe wa malaika watatu ulikuwa utolewe, mawazo ya waumini yalipaswa yaelekezwe katika hekalu la mbinguni, ambapo Kristo aliingia kufanya upatanisho kwa ajili ya watu wake. Matengenezo ya Sabato yalipaswa yaendelezwe. Ufa uliowekwa katika sheria ya Mungu sharti uzibwe. Sharti ujumbe utolewe kwa sauti kuu, ili wakazi wote wa dunia wapokee onyo. Lazima watu wa Mungu wasafishe roho zao kwa kuitii kweli, kisha waweze kusimama bila ya hatia mbele zake ajapo.Mar 61.3

    Kama Waadventista, baada ya mvunjiko mkuu wa matumaini wa mwaka 1844, wangeshikilia imani yao, na kufuata kwa umoja kabisa kufunguliwa kwa kipaji cha Mungu, kupokea ujumbe wa malaika watatu na katika uwezo wa Roho Mtakatifu kuutangaza kwa dunia, Bwana angetenda makuu akiongezea katika jitihada zao, kazi ingekuwa imemalizika, na Kristo angekuwa amekuja bila kuchelewa na kupokea watu na kuwapeleka katika zawadi yao.Mar 61.4

    Lakini katika kipindi hiki cha wasiwasi na kutokuwa na uhakika ambacho kilikuja mara baada ya kukata tamaa, waumini wengi wa Kiadventista waliiacha imani yao. . . Hivyo kazi ilizuiwa, na dunia iliachwa gizani. . .Mar 61.5

    Kwa muda wa miaka arobaini kutokuamini, manung’uniko, na uasi uliwafungia Israeli wa zamani nje ya nchi ya Kanaani. Dhambi za aina hiyo hiyo zimewachelewesha Israeli wa sasa wasiingie katika Kanaani ya mbinguni. Ahadi za Mungu hazikuwa na makosa katika nyakati zote hizi tofauti. Ni kutokuamini, kupenda dunia, kutojitoa na ugomvi kati ya wale wanaojiita watu wake Bwana ndivyo vimetuweka katika dunia hii ya dhambi na huzuni kwa miaka mingi hivi.Mar 61.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents