Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wanyenyekevu Watangaza Ujumbe, Sura ya 9

  Nasi tunalo lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu. 2 Petro 1:19.Mar 17.1

  Ujumbe huu [Utu 14:6,7] unatamkwa kuwa sehemu ya “injili ya milele.” Kazi ya kuhubiri injili haijakabidhiwa kwa malaika, lakini imekabidhiwa kwa watu. Malaika watakatifu ambao wamepewa jukumu la kuongoza kazi hii, wanasimamia msukumo mkuu kwa ajili ya wokovu wa watu; lakini uhubiri halisi wa injili linafanywa na watumishi wa Kristo hapa duniani.Mar 17.2

  Watu waaminifu, waliokuwa watiifu kwa maongozi ya Roho wa Mungu na mafundisho ya neno lake, walikuwa watangaze onyo hili kwa ulimwengu. Hawa ni wale ambao walikuwa wamezingatia “neno la unabii lililo imara zaidi,” ... “:Taa ing’aayo mahali penye giza, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka.” 2 Pet. 1:19. Hawa ni wale ambao walikuwa katika kufatuta maarifa ya Mungu kuliko hazina iIiyositirika, wakilihesabu neno hili kuwa “bora kuliko biashara ya fedha, na faida yake kuliko dhahabu safi.” Mith. 3:14. Bwana naye akawafunulia mambo makuu ya ufalme. “sifa ya BWANA iko kwao wamchao, naye atawajulisha agano lake.” Zab. 25:14.Mar 17.3

  Wanatheolojia wasomi hawakuuelewa ukweli, na hivyo hawakushiriki katika kuihubiri. Kama hawa wangekuwa walinzi waaminifu, wakiyachunguza Maandiko kwa bidii na kwa maombi, wangeujua wakati wa usiku; unabii ungewafungulia matukio yanayokuja. Lakini hawakuchukua nafasi hii na ujumbe ukatolewa na watu waliokuwa wanyenyekevu. Yesu alisema, “enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza.” Yn 12:35. Wale wanaoipa nuru migongo yao, nuru ambayo Mungu ameitoa, au wale wanaodharau kuitafuta hali ikiwa inapatikana, wanasalia gizani. Lakini Mwokozi anatamka: “Yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.” Yn. 8:12. Yeyote mwenye kusudi thabiti la kutafuta mapenzi ya Mungu, akikubali kwa dhati nuru ambayo tayari imetolewa, atapokea nuru kuu zaidi; kwa ajili ya roho hii moja nyota yenye nuru ya mbinguni itatumwa kuongoza katika kweli yote.Mar 17.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents