Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kiwango Uwezacho Kukiamini, Sura ya 86

  Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuzipinga hila za Shetani. Waefeso 6:11.Mar 94.1

  Katika kila uamsho wa kazi ya Mungu, mfalme wa giza husisimuliwa kwa ajili ya kushughulika zaidi; sasa yu katika kuweka juhudi ya juu zaidi kwa ajili ya pambano dhidi ya Kristo na wafuasi wake. Udanganyifu mkuu wa mwisho unakaribia kuonekana mbele zetu. Mpinga Kristo anaelekea kufanya matendo yake ya ajabu mbele zetu. Yaliyo bandia yatafanana sana na kweli, kiasi ambacho itakuwa vigumu kutofautisha kati ya hayo isipokuwa kwa kutumia Maandiko Matakatifu. Sharti kila kauli na kila muujiza vipimwe kwa shuhuda zake...Mar 94.2

  Ni wale tu ambao wameimarisha mawazo katika kweli za Biblia watakaoweza kusimama hadi kilele cha pambano kuu la mwisho. Kwa kila roho kutakuja jaribio la kujichunguza: Je, nitamtii Mungu kuliko wanadamu? Saa ya maamuzi ni hii. Je, miguu yako imewekwa juu ya mwamba wa neno la Mungu lisilobadilika? Je, tumejiandaa kusimama imara katika kutetea amri za Mungu na imani ya Yesu?. . .Mar 94.3

  Ni wajibu wa kwanza na wa juu zaidi wa kila kiumbe mwenye busara kujifunza ukweli toka kwa Maandiko, na kisha kutembea katika nuru, na kutia moyo wengine kufuata mfano wake. Siku kwa siku tunapaswa kusoma Biblia kwa bidii, hali tukipima kila wazo, na kulinganisha andiko kwa andiko. Kwa msaada wa mbingu tunapaswa kuwa na misimamo yetu kulingana na jinsi tutakavyojibu wenyewe mbele za Mungu. . .Mar 94.4

  Yesu aliahidi wanafunzi wake: “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.” Yn. 14:26. Lakini yapasa mafundisho ya Kristo yawe kwanza yamehifadhiwa mawazoni, ili Roho wa Mungu atukumbushe wakati wa hatari...Mar 94.5

  Wakati wa jaribio utakapofika, wale ambao wamefanya neno la Mungu kuwa kanuni yao ya maisha watafunuliwa. . . Hebu acha mateso yaanze, na wale walio katika imani nusu nusu na hali wakiwa wanafiki watayumba na kuiacha imani; lakini Mkristo wa kweli atasimama imara kama mwamba, imani yake ikiwa imara, tumaini lake likiwa pevu zaidi, kuzidi siku za neema.Mar 94.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents