Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Raia wa Mbinguni, Sura ya 67

    Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Waefeso 2:19.Mar 75.1

    Yesu anasema: “Tazama, Naja upesi.” Tunapaswa kuweka haya maneno mioyoni, na kutenda kama tunaoamini kwa kweli ya kwamba ujio wa Bwana u karibu, na ya kwamba sisi tu wasafiri na wageni hapa duniani.Mar 75.2

    Kila njia ya neema inapaswa kutumiwa vema na kwa uangalifu ili upendo wa Mungu upate kudumu rohoni zaidi na zaidi, “mpate kuyakubali yaliyo mema; ili mpate kuwa na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo: hali mmejazwa matunda ya haki.” Maisha yako ya Kikristo yapaswa kuchukua sura mpya ya juhudi na ufuasi hodari. Waweza kufikia kiwango cha juu kilichowekwa mbele yako kupitia kwa Maandiko, na sharti ufikie hapo kama unataka kuwa mtoto wa Mungu. Huwezi kubaki umesimama tu; ni lazima ama uende mbele au urudi nyuma. . .Mar 75.3

    Je, utabaki kuwa Mkristo uliyedumaa, au utafanya maendeleo yenye afya katika maisha yako ya kiroho? PaIipo na afya ya kiroho kuna ukuaji pia. Mtoto wa Mungu hukua hadi kufikia katika kimo kamili cha mwanamume au mwanamke katika Kristo. Hakuna kizuizi cha maendeleo katika suala hili. . .Mar 75.4

    Baadhi ambao wanapaswa kuwa na nguvu na msimamo katika Kristo bado wako kama watoto katika uwezo wao wa kuelewa na ufahamu utokanao na uzoefu wa kazi za Roho wa Mungu. Baada ya miaka ya uzoefu kupita, wameweza kuelewa kanuni za awali tu za mfumo mkuu wa imani na mafundisho yanayojenga dini ya Kikristo. Hawaelewi ukamilifu wa tabia ambao ndiyo unaopelekea katika kusifiwa kwa maneno “Umetenda vema...”Mar 75.5

    Tunaweza kupata ushindi mkuu, na tuna mbingu ya kupoteza kama tusipoupata ushindi huu. Moyo wa dhambi lazima usulubishwe; kwani ni kawaida yake kuwa katika machafuko ya maadili, na mwisho wake ni mauti... Omba ya kwamba uwezo mkubwa wa Roho Mtakatifu.... ushuke kama mshtuko wa umeme kwa roho iliyopooza, ili usababishe kila neva ishangilie kwa uhai mpya, ukimrejesha mtu toka katika hali ya hisia za kidunia zilizokufa, hadi kwa hali ya kiroho iliyo na nguvu. Kwa namna hiyo mtakuwa washiriki pamoja na uwezo wa kimbingu... na katika roho zenu kutaakisiwa sura yake ambaye kwa kupigwa kwake mmeponywa.Mar 75.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents