Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kumjua Mungu Kikamilifu, Sura ya 68

    Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Yohana 17:3.Mar 76.1

    Njia moja pekee ya kuwa tayari kwa ajili ya kuja kwake ni kumjua Mungu. . . Lakini wengi wa wale wanaodai kumwamini Kristo hawamjui Mungu. Dini yao ni ya juu juu tu. Hawampendi Mungu; hawajifunzi tabia yake; kwa hiyo, hawajui namna ya kutegemea, hawajui jinsi ya kutazama na kuishi. Hawajui maana ya upendo wenye pumziko, au kile kinachomaanishwa na kutembea kwa imani.... Wanashindwa kuelewa ya kwamba ni wajibu wao kupokea, ili kufaidisha wengine.Mar 76.2

    Kulingana na hekima yake, dunia haimjui Mungu. Wengi wamemnena Yeye kwa ufasaha, lakini mawazo yao hayawaleti watu karibu zaidi naye, kwa sababu wao wenyewe hawapo katika muunganiko wenye nguvu na Yeye. Hali wakijidai kuwa na hekima, hujikuta wakiwa wapumbavu. Ujuzi wao wa Mungu una mapungufu.Mar 76.3

    Hatuwezi kumpata Mungu kwa utafiti, lakini amejifunua mwenyewe katika Mwana wake, ambaye ni mng’ao wa utukufu wa Baba na dhihirisho la taswira ya nafsi yake. Kama tunatamani ufahamu wa Mungu sharti tuwe kama Kristo. . . Kuishi kwa imani maisha yaliyo safi katika Kristo kama Mwokozi wetu binafsi kutaleta kwa muumini ufahamu ulio wazi zaidi na wa juu kuhusu Mungu.Mar 76.4

    Kristo ndiye ufunuo wa Mungu ulio kamili zaidi. “Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote,” anasema; “Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.” Ni kwa kumjua Kristo tu ndipo twaweza kumjua Mungu. Kadiri tunavyomjua Yeye, tunabadilishwa na kufanana naye, tukiandaliwa kukutana naye ajapo...Mar 76.5

    Sasa ndiyo wakati wa kujiandaa kwa ajili ya ujio wa Bwana. Utayari wa kumpokea hauwezi kupatikana kwa sekunde moja. Maandalizi kwa ajili ya tukio hili la heshima kuu sharti yapelekane na subira yenye hadhari na kungoja, vikiunganika na kazi itendwayo kwa moyo. Kwa hiyo watoto wa Mungu wanamtukuza Yeye. Kati ya mazingira ya shughuli nyingi za maisha, sauti zao zitasikika zikiongea maneno ya kutia moyo, tumaini, na imani. Vyote walivyo navyo, na wao wenyewe vimewekwa wakfu kwa ajili ya utumishi wa Bwana. Kwa namna hiyo, wanajiandaa kukutana na Bwana wao; na hapo atakapokuja, watasema kwa furaha, “Huyu ndiye Mungu wetu; tuliyemngoja, ili atuokoe. . . tutafurahia na kushangilia wokovu wake.”Mar 76.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents