Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Utakaso wa Kibiblia Wafafanuliwa, Sura ya 81

    “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.” Yohana 17:17Mar 89.1

    Wale wanaotakaswa kupitia kwa ile kweli ni shuhuda zilizo hai za uwezo wake, na wawakilishi wa Bwana aliyefufuka. Dini ya Kristo itasafisha mionjo, itatakasa maamuzi, itainua, itachuja, na kuadilisha roho, ikimfanya Mkristo kuwa tayari zaidi kwa ajili ya jumuiya ya malaika wa mbinguni.Mar 89.2

    “Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.” Yn. 17:19. “Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo.” I Pet. 1:22. “. . .kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.” 1 Kor. 7:1. . .Mar 89.3

    Hapa ndipo ulipo utakaso wa Biblia. Siyo tu kazi ya kujionesha nje au kazi ya nje. Huu ni utakaso uliopokelewa kupitia kwa mfereji wa ukweli. Ni kweli iliyopokelewa ndani ya moyo, na kuonekana katika matendo halisi ya maisha.Mar 89.4

    Hakuna utakaso wa Kibiblia kwa wale ambao wanaitupa sehemu ya kweli nyuma yao. Katika neno la Mungu ipo nuru ya kutosha, kiasi kwamba hakuna anayehitaji kukosea.. .Yesu, ambaye alifikiriwa kama mwanadamu, alikuwa mkamilifu, lakini bado alikuwa katika neema. “Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.” Lk 2:52. Hata Mkristo aliye kamili sana aweza kuongezeka kwa kudumu katika ufahamu na upendo wa Mungu. . .Mar 89.5

    Utakaso si kazi ya wakati mfupi au saa moja, au siku moja. Ni ukuaji katika neema unaoendelea, . . Shetani yuko hai, na anatenda kazi, na kila siku tunahitajika kulia kwa Mungu kwa udhati kabisa kwa ajili ya msaada na nguvu za kumpinga. Kadiri Shetani anavyoendelea kutawala tutakuwa na kazi ya kutiisha nafsi, makosa ya kushinda, na hakuna mahali pa kukoma, hakuna hatua tutakayofikia na kusema tumeshafika. . .Mar 89.6

    Daima maisha ya Kikristo ni mwendo unaoendelea. Yesu anaketi kama msafishaji na mtakasaji wa watu wake; na sura yake inapokuwa imeakisiwa kikamilifu ndani yao, wanakuwa wakamilifu na watakatifu, na huwa tayari kwa ajili ya kubadilishwa.Mar 89.7

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents