Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kwa nini Wasiofanya Kazi ni Wengi Hivyo, Sura ya 115

  Nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. Matendo 1:8.Mar 123.1

  Waumini katika kila kizazi wana sehemu katika dhamana waliyopewa wale wanafaunzi wa kwanza. Kila aliyepokea injili amepewa ukweli mtakatifu wa kutoa kwa ulimwengu. Watu wa Mungu walio waaminifu wamekuwa wamishonari wenye ari siku zote huku wakiweka wakfu raslimali zao kwa ajili ya heshima yajna lake, na kutumia talanta zao kwa busara katika huduma yake. . .Mar 123.2

  Washiriki wa kanisa la Mungu wanapaswa kuwa na ari katika kutenda mema. Wanapaswa kuwahudumia wale wanaohitaji msaada kwa mioyo iliyojaa huruma, na kuwafanya wenye dhambi waujue upendo wa Mwokozi. Kazi kama hiyo mahitaji juhudi kubwa, lakini huwa ina manufaa makubwa. Wale wanaoifanya kwa nia ya dhati wataona roho zikiongolewa na kuja kwa Mwokozi. . .Mar 123.3

  “Na Roho na bibi arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo!” Ufu. 22:17. Agizo la kutoa mwaliko huu unajumuisha kanisa lote. Kila aliyeusikia mwaliko anapaswa kuurudia ujumbe toka kwenye kilima na bondeni akisema, Njoo!....Mar 123.4

  Mamia kwa maelfu ambao wamesikia ujumbe wa wokovu, bado hawafanyi cho chote katika masoko, wakati walitakiwa kujishughulisha na aina fulani ya huduma. Watu kama hao Kristo anawaambia, “Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?” kisha, anaendelea kusema, “Enendeni nanyi katika shamba la mizabibu.” Mat. 20:6,7. Inakuwaje watu wengi zaidi hawaitikii wito huo? Je, kwa sababu wanadhani kwamba hawahusiki kwa kuwa huwa hawasimami mimbarani? Wanapaswa kujua kwamba kuna kazi kubwa nje ya mimbara, kufanywa na maelfu ya washiriki waliojitoa.Mar 123.5

  Mungu amekuwa akisubiri kwa muda mrefu roho ya huduma ilijaze kanisa lote ili kila mtu amtumikie kulingana na uwezo wake. Washiriki wa kanisa la Mungu wanapofanya kazi waliyopewa katika maeneo yenye uhitaji nyumbani na katika nchi za mbali, katika kutimiza agizo la injili, ulimwengu mzima utaonywa haraka, na Bwana yesu atarudi hapa duniani kwa nguvu na utukufu mkuu. “Habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho makapokaja.Mar 123.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents