Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kubatilishwa kwa Sheria ya Mungu Nchini Marekani, Sura ya 171

  Wakati umewadia BWANA atende kazi; kwa kuwa wameitangua sheria yako. Zaburi 119:126.Mar 179.1

  Wakati unakuja ambapo sheria ya Mungu, kwa namna ya pekee, itafanywa kuwa batili katika nchi yetu [Marekani]. Watawala wa taifa letu, watashinikiza sheria ya Jumapili, kwa kutumia maagizo ya mabaraza ya kutunga sheria, na kwa namna hiyo watu wa Mungu watafikishwa katika hatari kuu. Wakati taifa letu kupitia kwenye mabaraza yake ya kutunga sheria, litakapopitisha sheria zinazotawala dhamiri kuhusiana na haki zao za kidini, wakishinikiza kuadhimisha Jumapili kama siku ya ibada, na wakati huo kuleta mamlaka inayokandamiza na kuwalemea wale wanaoishika Sabato ya siku ya saba na maazimio na makusudi yake, sheria ya Mungu itabatiIishwa katika nchi.Mar 179.2

  Wakati nchi hii ambayo Bwana aliitoa kama kimbilio kwa watu wake, ili wapate kumwabudu kulingana na matakwa ya dhamiri zao wenyewe, nchi ambayo kwa miaka mingi ngao ya uwepo wake imeenea, nchi ambayo Mungu ameipendelea kwa kuifanya kuwa bohari la dini safi ya Kristo-wakati nchi hii itakapokana kanuni za Kiprotestanti kupitia kwa vyombo vyake vya kutunga sheria, na hivyo kutoa uso wake kwa uasi wa Kirumi katika kuharibu sheria ya Mungu — ndipo hapo ile kazi ya mwisho ya mtu wa dhambi itakapofunuliwa. Waprotestanti watabwaga mvuto wao wote na nguvu upande wa Upapa; kwa sheria ya kitaifa inayosimika sabato ya uongo, wataihuisha na kuipa nguvu imani potofu ya Rumi, hali wakiufufua udhalimu na udhalilishaji wake wa dhamiri. Huo ndiyo utakao kuwa wakati kwa ajili ya Mungu kutenda kazi kwa uwezo mkubwa kuithibitisha kweli yake.Mar 179.3

  Nabii anasema: “Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umenguka umeanguka Babeli ule mkuu... Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.” Je, dhambi zake zinafika hadi mbinguni lini? Wakati wanapofikia hatima ya kuibatilisha sheria ya Mungu kwa kutunga sheria yao. Ukomo wa mwanadamu ni fursa yake katika kuonesha kwamba ni nani aliye mtawala wa mbingu na nchi. Nguvu ya Shetani inapokusanya chembechembe zinazotoka chini, Mungu atatuma nuru na uwezo kwa watu wake, ili ujumbe wa kweli utangazwe kwa ulimwengu wote.Mar 179.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents