Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kipindi Nyeti. Sura ya 32

  Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo. Malaki 3:2.Mar 40.1

  Kwa sababu ya dhambi zao, wana wa Israeli walizuiwa kuukaribia mlima siku ile Bwana alipokuwa anashuka kuja kuitangaza sheria yake, ili wasiteketezwe kwa utukufu unaochoma wa kuwepo kwake. Kama udhihirisho wa aina hiyo ulionekana mahali palipochaguliwa kwa ajili ya kuitangaza sheria yake, mahakama yake itakuwa ya kutisha zaidi siku atakapokuja kuhukumu kwa sheria hizo takatifu. Wale walioikanyaga mamlaka yake watawezaje kustahimili utukufu wake katika siku ile ya ghadhabu ya mwisho?Mar 40.2

  Uwepo wa Mungu ulipodhihirishwa katika Mlima wa Sinai, utukufu wa Mungu ulikuwa kama moto ulao. . . Lakini siku atakapokuja Yesu katika utukufu, pamoja na malaika wake watakatifu dunia yote itang’aa kwa nuru kali ya kuwepo kwake.Mar 40.3

  Tangu kuwepo kwa mwanadamu, hakujawahi kushuhudiwa uweza wa Mungu kama ule ulioonekana siku ile sheria ilipotangazwa.... Katikati ya msukosuko mkubwa wa vitu vya asili, sauti ya Mungu ilisikika kama tarumbeta kutoka katika lile wingu. Mlima ulitikiswa tangu chini hadi kileleni, na jeshi la Israeli, wakitetemeka kwa hofu, walianguka chini kifudifudi. Yule ambaye wakati huo sauti yake iliitikisa dunia amesema, “Mara moja tena nitatetemesha si nchi tu, bali na mbingu pia.”Mar 40.4

  Musa alipotoka mbele ya uso wa Mungu kule mlimani, baada ya kupokea mbao za ushuhuda, wana wa Israeli waliokuwa na hatia hawakuweza kustahimili nuru iliyong’aa usoni pake. Wakosaji hawataweza kabisa kumwangalia Mwana wa Mungu atakapokuja katika utukufu wa Baba yake, akizungukwa na jeshi lote la mbinguni, akija kutoa hukumu kwa wale walioivunja sheria yake na kuukataa upatanishao wake. . .Mar 40.5

  Lakini katika tufani ya mapigo ya Mungu, watoto wa Mungu hawatakuwa na sababu ya kuogopa. “Bwana atakuwa kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli.” Siku itakayokuwa ya kutisha na maangamizi kwa walioiasi sheria ya Mungu, itakuwa ya “furaha isiyoneneka, yenye utukufu,” kwa wale watii.Mar 40.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents