Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ghadhabu ya Mungu Katika Nchi, Sura ya 17

  Watu wakivunjika moyo kwa hofu, na kwa kuyatazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Luka 21:26.Mar 25.1

  Laiti watu wa Mungu wangejua uharibifu unaoyajia maelfu ya miji, ambayo sasa imezama katika ibada ya sanamu!. . .Mar 25.2

  Muda si mrefu niliona taswira ya ajabu. Niliona tufe la moto likianguka kati ya majengo mazuri, na kuyaharibu palepale. Nilisikia mtu akisema, “tulijua kuwa ghadhabu ya Mungu ilikuwa inaijia dunia, lakini hatukujua kuwa ingekuja mapema hivi.” Wengine walisema, “Ninyi mlikuwa mnajua, kwa nini hamkutuambia? Sisi hatukujua.” Kila upande niliskia maneno kama hayo yakisemwa. . .Mar 25.3

  Hivi karibuni matatizo makubwa yatatokea katika mataifa—matatizo hayo hayataisha mpaka Yasu atakaporudi. Tunahitaji kujitahidi kwa pamoja kuliko wakati mwingine wo wote ule, tukimtumikia Yeye aliyeandaa kiti chake cha enzi kule mbinguni na ambaye utawala wake utakuwa juu ya wote. Mungu hajawaacha watu wake, na nguvu yetu iko katika kutokumwacha.Mar 25.4

  Ghadhabu ya Mungu iko katika nchi hii. Vita na tetesi za vita, majanga ya moto na mafuriko, yanaashiria wazi wazi kipindi cha dhiki kimekaribia, dhiki ambayo itazidi kuongezeka hadi mwisho. Hatuna muda wa kupoteza. Dunia imejaa roho ya vita. Unabii wa sura ya 11 ya kitabu cha Danieli umekaribia kufikia utimilifu wake wa mwisho....Mar 25.5

  Ijumaa iliyopita asubuhi, muda mfupi kabla sijaamka, taswira ya ajabu ilipita mbele yangu. Niliona kana kwamba nilikuwa naamka kutoka usingizini lakini sikuwa nyumbani kwangu. Kutoka katika madirisha niliona moto mkubwa. Matufe makubwa ya moto yalikuwa yakiziangukia nyumba, na mishale ya moto ilikuwa ikiruka kutoka katika nyumba hizi kuelekea kila upande. Ilikuwa vigumu kuidhibiti mioto iliyokuwa ikiwaka, na nyumba nyingi zilikuwa zinateketea. Hofu waliyokuwa nayo watu ilikuwa haielezeki.Mar 25.6

  Miji iliyo katika mataifa itashughulikiwa kwa uhakika, lakini haitaadhibiwa kwa hasira yote ya Mungu, kwa kuwa roho kadhaa zitakuwa zimejinasua kutoka kwa yule adui, na zitatubu na kuongolewa, wakati waliobaki watakuwa wakijawa na hasira dhidi ya siku ile ghadhabu.Mar 25.7

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents