Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jukumu la Umizimu Katika Udanganyifu, Sura ya 158

    “Wapenzi msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani” 1 Yohana 4:1.Mar 166.1

    Wengi watanaswa mtegoni kupitia fundisho kwamba umizimu ni ujanja wa kibinadamu; wanapokabiliwa ana kwa ana na matukio wasiyoweza kuyaelewa ila kukiri tu kwamba ni muujiza, nao watadanganyika, wakiyakubali kama uwezo mkuu wa Mungu.Mar 166.2

    Kadiri mafundisho ya umizimu yanavyopokelewa makanisani, ustahimilivu uliowekwa kwenye moyo wa mwanadamu utaondolewa, na kukiri kuwa muumini wa dini litakuwa vazi la nje kufunika uovu mkuu. Kuamini mafunuo ya kimizimu hufungua mlango kwa roho zidanganyazo na mafundisho ya mwovu, na hivyo mvuto wa malaika waobu kutawala makanisani.Mar 166.3

    Mahubiri ya kutafuta umashuhuri hayawezi kupinga umizimu. Hayana ngao kukinga watu wake dhidi ya mvuto wake mwovu wa kupindukia. Lawama dhidi ya athari mbaya ya umizimu itawaangukia wahubiri wa kizazi kipya; kwani wameikanyaga kweli miguuni mwao, na badala yake wamefurahia hekaya.Mar 166.4

    Shetani kwa muda mrefu amekuwa akijiandaa kufanya mashambulizi yake ya mwisho ya kuudanganya ulimwengu. Misingi ya kazi yake iliwekwa kwa usadikisho aliopatiwa Hawa pale Edeni: “Hakika hutakufa.” “Kwa maana Mungu anajua kuwa ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” Mwa. 3:4, 5. Taratibu lakini kwa hakika Shetani ameandaa udanganyifu wake mkuu kupitia imani ya umizimu. Hajafaulu kikamilifu kama alivyokusudia; ila lengo lake IitatimiIika mnamo kipindi cha mwisho wa nyakati. Nabii asema: “Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote; kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.”Ufu. 16:13, 14. Isipokuwa kwa wale wenye ulinzi wa Mungu, kupitia imani katika Neno lake, ulimwengu wote utatekwa na udanganyifu wake. Watu wanapumbazwa kwa usalama bandia, nao watazinduliwa tu na umwagwaji wa hasira za Mungu.Mar 166.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents