Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Je, Kuna Sanamu Zozote Hapa?, Sura ya 40

  Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu. 1 Yohana 5:21Mar 48.1

  Kila mtoto wa Mungu atachekechwa kama ngano, na katika mchakato wa kuchekechwa, kila aina ya anasa inayopendwa ambayo inapotosha mawazo toka kwa Mungu lazima itolewe. Katika familia nyingi rafu za vitabu na vimeza vya magazeti, kumejazwa mapambo na picha...Hivyo mawazo, ambayo yanapaswa kuwa katika neno la Mungu katika shauku ya mambo ya kimbingu, yanashushwa chini kwa vitu vya kawaida. Je, hiki siyo kisehemu cha ibada ya sanamu? Je, siyo bora kwa fedha ambayo imetumika kwa namna hiyo ingetumika kubariki watu, kupunguza makali ya mateso, kuvisha walio uchi, na kulisha wenye njaa? Je, isiwekwe katika hazina ya Bwana ili kuendeleza kusudi lake na kujenga ufalme wake duniani?Mar 48.2

  Suala hili lina umuhimu mkuu, na linasisitizwa kwako ili kukuokoa toka katika dhambi ya ibada ya sanamu. Baraka zingekuja kwa roho zenu kama mngetii neno lililonenwa na Mtakatifu wa Israeli, “Msiwe na miungu mingine ila mimi.” Wengi wanajiongezea taabu zisizo za lazima na wasiwasi kwa kutumia muda na mawazo kwa ajili ya mapambo yasiyo ya lazima ambayo huzijaza nyumba zao. Nguvu ya Mungu inahitajika ili kuwainua toka katika upenzi huu; kwani ibada ya sanamu imo katika makusudio yote na dhamira zao.Mar 48.3

  Yeye achunguzaye mioyo, anatamani kuwaongoa watu wote toka katika kila aina ya ibada ya sanamu. Hebu Neno la Mungu, kitabu cha uzima chenye baraka, kichukue nafasi katika meza ambazo sasa zimejazwa na mapambo. Tumia pesa yako katika kununua vitabu ambavyo vitakuwa ni njia ya kuelimisha mawazo yako kulingana na ukweli wa leo... Kamata Neno la Bwana kama hazina ya hekima na upendo; hiki ni kitabu ambacho ni Mwongozo uelekezao katika njia ya kwenda mbinguni. . .Mar 48.4

  Laiti mngechunguza Maandiko mioyo ikiwa katika sala, huku roho zikiwa zimetolewa kwa Mungu! Laiti mngechunguza mioyo yenu mkiwa na mishumaa inayowaka, na kugundua na kuvunja kamba zinazoonekana kuwa imara kabisa zikiwafunga na mazoea ya kidunia, ambayo yanapotosha mawazo toka kwa Mungu! Msihi Mungu ili akuoneshe kila aina ya mazoea ambayo huvuta mawazo yako na matashi yako mbali na Yeye. Mungu amempatia mwanadamu sheria takatifu kama kipimo chake cha tabia. Kwa sheria hii waweza kuona na hatimaye kushinda kila upungufu uliopo katika tabia yako. Waweza kujiengua mwenyewe kutoka katika kila sanamu, na kujiunganisha na kiti cha enzi cha Mungu kwa mnyororo wa dhahabu wa neema na kweli.Mar 48.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents