Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Hatari za Sayansi Isiyo ya Kweli, Sura ya 126

    Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo. 1 Timotheo 6:20.Mar 134.1

    Kule New Hampshire walikuwepo wale ambao walikuwa wakifanya kazi ya kusambaza dhana za uongo kuhusu Mungu. Nilipewa nuru ya kwamba watu hawa walikuwa wakifanya kweli isiwe na mguso kwa kutumia dhana zao, baadhi ya dhana hizo zikipelekea katika mapenzi - huru. Nilioneshwa kwamba watu hawa walikuwa wakishawishi roho kwa kuwasilisha dhana zitokanazo na makisio yao kuhusu Mungu...Mar 134.2

    Kati ya mitazamo mingine waliyokuwa nayo, ni kwamba wale ambao walipata kutakaswa wasingeweza kutenda dhambi, na mtazamo huu waliuwasilisha kama ndicho chakula cha kiinjili. Nadharia zao zisizo za kweli, zikiwa na mzigo wa mvuto wa udanganyifu, zilikuwa zikiwaharibu wao wenyewe na wengine kwa kiasi kikubwa. Zilikuwa zikiongezeka katika mwonekano wa kiroho kwa wale ambao hawakuweza kuona uovu wa nadharia hizi zilizokuwa zimevishwa mwonekano mzuri. Uovu mkuu ulikuwa umetokea tayari. Fundisho ya kwamba wote ni watakatifu lilikuwa limepelekea kwa imani kwamba mapenzi ya waliotakaswa hayakuwaweka katika hatari ya kupotoka. Matokeo ya imani hii yalikuwa ni utimilifu wa tamaa hizi mbovu mioyoni ambazo, ingawa zilidaiwa kutakaswa, zilikuwa mbali na usafi wa mawazo na matendo.Mar 134.3

    Hili ni moja tu ya yale ambayo niliitwa kukemea kwa wale waliokuwa wakiwasilisha fundisho la mungu asiye na hisia aliyechangamana na viumbe vya asili, na fundisho la mwili mtakatifu.Mar 134.4

    Siku zijazo, kweli kaharibiwa uhalisia wake kwa kubadilishwa na kanuni za watu. Nadharia zinazodanganya zitawasilishwa kama mafundisho yaliyo salama. Sayansi isiyo ya kweli ni moja ya mawakala wa Shetani alizozitumia katika nyua za mbinguni, na anaendelea kuitumia leo...Mar 134.5

    Ninawasihi wale wafanyao kazi kwa ajili ya Mungu wasikubali kilicho bandia badala ya kile kilicho halisi. Tunayo Biblia nzima ambayo imejaa ukweli wa thamani. Hatuhitaji kuwa na makisio au misisimko itokanayo na uongo. Katika chetezo cha kweli, kama inavyowasilishwa katika mafundisho ya Kristo, tunacho kile ambacho kitasadikisha na kuongoa roho. Wasilisha zile kweli alizokuja kuzitangaza Kristo hapa duniani katika urahisi na nguvu ya ujumbe unaoutoa utahisika wenyewe. Usiwasilishe nadharia au majaribio ambayo hayana msingi katika Biblia.Mar 134.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents