Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Vyakula na Ardhi Katika Siku za Mwisho, Sura ya 173

    Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake. Mathayo 6:34.Mar 181.1

    Bwana amenionesha katika njozi, kwa kurudia rudia, ya kwamba ni kinyume cha Biblia kujilimbikizia mahitaji ya kimwili kwa ajili ya wakati wa taabu. Nilioneshwa ya kwamba kama watakatifu watakuwa wamejiwekea chakula, hata katika mashamba yao, wakati wa taabu, ndipo upanga, njaa na maafa vitakapokuwepo katika nchi, watu wenye mikono yenye vurugu watawanyang’anya na wageni watavuna mashamba yao. Ndipo kwetu sisi, huo utakuwa wakati wa kumtegemea Mungu kikamilifu, naye atatutunza. Niliona ya kuwa tutahakikishiwa mkate na maji wakati huo, na hatutapungukiwa wala kufa njaa. Bwana amenionesha ya kwamba baadhi ya watoto wake wataogopa watakapoona bei za vyakula zikipanda, na watanunua chakula na kukitunza kwa ajili ya wakati wa taabu. Kisha wakati wa hitaji, niliona wakienda walipohifadhia chakula na walipokitazama walikuta minyoo, na viumbe hai waliojaa, na hakikufaa kwa matumizi.Mar 181.2

    Nyumba na ardhi havitakuwa na thamani kwa watakatifu wakati huo wa taabu kuu, kwani itawapasa kukimbia mbali na makundi ya watu walioghadhibika, na pia wakati huo mali zao hazitauzwa ili kuendeleza msukumo wa ukweli wa leo. . .Mar 181.3

    Niliona ya kuwa kama wapo ambao watang’ang’ania mali zao na hawatamuuliza Bwana wazifanyie nini, hatawafanya wajue wajibu wao na wataruhusiwa kutunza mali zao, kisha wakati wa taabu mali itainuka juu dhidi yao kama mlima ulio tayari kuwaangukia na kuwasaga na watajaribu kuugawa, lakini hawataweza. . . . Lakini kama wangetamani kufundishwa, angewafundisha, wakati wa hitaji, wakati gani wa kuuza na kiasi gani cha kuuza wakati wa taabu.Mar 181.4

    Wakati wa pambano kuu dhidi ya Shetani wale walio watii kwa Mungu wataona kila namna ya kuungwa mkono na dunia ikikatika. Kwa sababu watakataa kuvunja sheria yake kwa kutii mamlaka ya kidunia, watazuiwa kuuza au kununua. Hatimaye itatamkwa ya kuwa wauawe. . . Lakini kwa wale walio watii ahadi hii inatolewa, “Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake, atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma Isa. 33:16. Watoto wa Mungu wataishi kwa ahadi hii.Mar 181.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents