Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Je, Utashinda Jaribio?,Sura ya 35

  Nawe utaikumbuka njia ile yote BWANA, Mungu wako, aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu, kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo. Kumbukumbu la Torati 8:2Mar 43.1

  Mungu atawajaribu watu wake.... Kama ule ujumbe [ujumbe wa mwaka 1844] ungekuwa wa muda mfupi kama wengi wetu tulivyodhani, kusingekuwa na muda wa kujenga tabia kwa ajili yao. Wengi walisukumwa na hisia, na wala si kanuni au imani, na ujumbe huu nyeti na wa kutisha uliwagusa. Uligusa hisia zao, na kuamsha hofu yao, lakini haukukamilisha kazi ambayo Mungu alikuwa amekusudia uifanye. . .Mar 43.2

  Mungu anawaongoza watu wake hatua kwa hatua. Huwa anawaleta mahali tofauti palipoktisudiwa kuonesha kile kilicho moyoni. Wengine wanastahimili mahali pamoja, lakini wanaanguka panapofuata. Katika kila hatua inayoongezeka moyo unajaribiwa na kupimwa kwa kina zaidi. Watu wa Mungu wakiona kuwa mioyo yao inapingana na kazi hii, wanapaswa kujua kuwa bado wana kazi ya kufanya ili washinde. . . Baadhi wako tayari kupokea kipengele kimoja: lakini Mungu anapowaletea kipengele kingine cha kuwajaribu, wananywea na kurudi nyuma, kwa kuwa wanaona kuwa kinagusa sanamu wanavoipenda. Hapa wana nafasi ya kuona kilicho ndani ya mioyo yao, kinachomzuia Yesu kuingia. Wanathamini kitu kingine kuliko ukweli, na mioyo yao haiko tayari kumpokea Yesu. Watu wanapimwa na kujaribiwa kwa muda mrefu kuona kama wataziacha sanamu zao. . . Wale watakaopita katika kila kipengele, na kushinda kila jaribu, bila kujali gharama, watakuwa wamefuata ushauri wa yule Shahidi wa Kweli, nao watapokea mvua ya masika, na kwa hiyo watakuwa wanafaa kunyakuliwa.Mar 43.3

  Mungu unawajaribu watu wake katika ulimwengu huu. . . Hapa, katika ulimwengu huu, katika siku hizi za mwisho, watu wataonesha ni nguvu gani inayogusa mioyo yao na kutawala matendo yao. Kama ni ile nguvu ya ukweli wa Mungu, itapelekea kwenye matendo mema. Itamwinua atakayeipokea, na kumfanya awe na moyo mwema, wenye ukarimu, kama alivyo Bwana wake wa mbinguni. . .Mar 43.4

  Vijana na wazee, Mungu anawajaribu sasa. Sasa hivi mnachagua hatima yenu ya milele.Mar 43.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents