Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wenye Busara au Wapumbavu?, Sura ya 46

    Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. Mathayo 25:1,2.Mar 54.1

    Hatupaswi kuridhika na wazo kwamba kwa sababu tu washiriki wa kanisa basi tumeokolewa, hali tukiishi bila kuonesha vithibitisho ya kwamba tumeambatana na mfano wa Kristo, hali tuking’ang’ania mazoea yetu ya kale, na kufuma vazi letu kwa nyuzi za dhana na desturi za kidunia. . .Mar 54.2

    Wanawali kumi wapo katika kukesha wakati wa jioni ya historia ya dunia hii. Wote wanadai kuwa Wakristo. Wote wanao wito, jina, taa, na wote wanadai kufanya huduma ya Mungu. Inavyoonekana, wote wanasubiri kuja kwake. Lakini watano wana upungufu. Watano watakutwa wakishangaa, wakiaibika, wakiwa nje ya ukumbi wa sherehe.Mar 54.3

    Tunawakilishwa ama na wanawali wenye busara au wapumbavu. Wapo wengi ambao hawatasalia miguuni pa Yesu, na kujifunza kwake. Hawana ujuzi wa njia zake; hawako tayari kwa ajili ya ujio wake. Wamekuwa wakijidai tu kumsubiri Bwana. Hawajawa katika kukesha na kuomba kwa imani ile itendayo kazi kwa upendo na kutakasa roho. Wamekuwa wakiishi maisha ya uzembe. Wameusikia ukweli na kuukubali, lakini hawajauweka katika matendo ya maisha ya kila siku. Mafuta ya neema hayajazi taa zao, na hivyo hawajajiandaa kuingia katika sherehe ya arusi ya Mwanakondoo.Mar 54.4

    Msiwe kama wanawali wapumbavu, ambao wanachukulia kwa urahisi kuwa ahadi za Mungu ni zao, wakati hawafuati sheria za Kristo. Kristo anatufundisha ya kwamba kukiri tu kwa maneno ni bure. “Mtu yeyote akitaka kumfuata,” anasema, “na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku anifuate.”. . .Mar 54.5

    Tunapokuwa tumepitia jaribio la Mungu katika mchakato wa kusafisha na kutakasa; wakati moto wa tanuru unapokuwa umechoma taka, na kisha tabia kama dhahabu ya kweli iliyosafishwa inapotokea, bado twaweza kusema, pamoja na Paulo, “Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; Bali nakaza mwendo ... ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.”Mar 54.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents