Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sauti Kuu Itakaposikika, Sura ya 19

  Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini. Warumi 13:11.Mar 27.1

  Mwisho umekaribia, ukitunyemelea kimya kimya kama ujio wa mwizi wakati wa usiku. Bwana atusaidie tusije tukalala kama wengine wanavyafanya, bali tukeshe na kuwa makini. Ukweli Utashinda hivi karibuni kwa utukufu, na wale wote ambao sasa wanachagua kuwa wafanyakazi pamoja na Mungu, watashinda pamoja nao. Muda ni mfupi: usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi. . .Mar 27.2

  Wakati unakuja ambapo kutakuwa na wengi wanaoongoka kwa siku kama ilivyokuwa siku ya Pentekoste, baada ya mitume kupokea Roho Mtakatifu. . .Mar 27.3

  Wengi wameuacha mwaliko wa Injili upite bila kuutii; wamejaribiwa sana lakini vikwazo kama milima vimekuwa vikionekana mbele ya nyuso zao, na kuwafanya wasisonge mbele. Kwa njia ya imani, saburi, na ujasiri, wengi watavivuka vikwazo hivi na kuingia katika mwanga wenye utukufu.Mar 27.4

  Vizuizi vimewekwa bila kujua katika ile njia nyembamba; mawe ya kujikwaa yamewekwa katika njia; haya yataondolewa. Kinga ambazo wachungaji wa bandia wamewazungushia kondoo wao zitaishiwa nguvu; wengi wataingia katika nuru, na kufanya kazi ya kuitangaza nuru. Viumbe wenye akili kutoka mbinguni wataungana na wajumbe wa kibinadamu. Likiwa limetiwa moyo kwa njia hiyo, kanisa litaondoka na kuangaza, Iikitumia nguvu zake zote takatifu katika shindano; kwa njia hiyo kusudi la Mungu litatimizwa; lulu zilizokuwa zimepotea zitakuwa zimepatikana....Mar 27.5

  Wakati wa sauti kuu, kanisa, likisaidiwa na majaliwa na kuingilia kati kwa Mungu wake aliyeinuliwa, litatoa elimu ya wokovu kwa wingi kiasi kwamba nuru itapelekwa katika kila jiji na kila mji. Dunia itajaa elimu ya wokovu. Kufanywa upya kwa njia ya Roho wa Mungu kutawapa mafanikio makubwa wale watakaokuwa wanajitahidi sana, ili nuru ya ukweli wa sasa ionekane iking’aa kila mahali.Mar 27.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents