Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Tabia Inayokubalika Mbinguni, Sura ya 75

    Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. 1 Timotheo 4:12.Mar 83.1

    Yesu, Mfalme wa mbinguni, ameachia vijana kielelezo. Alifanya kazi ngumu katika karakana ya Nazareti kwa ajili ya chakula chake cha kila siku. Alikuwa mtiifu kwa wazazi wake, na hakujichukulia mamlaka ya matumizi ya muda na hata hakupenda kufanya mambo kulingana na mapenzi yake mwenyewe. Kamwe kijana hawezi kupata mafanikio ya kweli kama mtu au Mkristo huku akiwa mwepesi kuendekeza tabia mbaya. Mungu hatuahidi starehe, heshima au utajiri katika huduma yake; lakini anatuahidi ya kuwa baraka zote tunazozihitaji zitakuwa zetu, “na udhia,” na katika dunia ijayo “uzima wa milele.” Kristo hatakubali chochote kilicho pungufu ya kujitoa kikamilifu kwa huduma yake. Hili ni somo ambalo kila mmoja wetu sharti ajifunze...Mar 83.2

    Tunavyo vielelezo dhahiri vya nguvu ya kanuni ya kidini iliyo imara... Tundu la simba lililokuwa wazi halikumzuia Danieli asisali kila siku, wala tanuru la moto halikumshawishi Shadraka na wenzake kuanguka mbele ya sanamu ambayo Nebukadneza aliisimamisha. Vijana walio na kanuni imara watakuwa radhi kuepuka anasa, kudharau maumivu, na kuwa jasiri hata mbele za tundu la simba na tanuru la moto ili tu wawe wakweli kwa Mungu. Angalia tabia ya Yusufu. Uadilifu lilijaribiwa katika kiwango cha juu sana, lakini ushindi wake ulikuwa kamili. Katika kila hatua kijana huyu mwadilifu alistahimili jaribu. Kanuni ile ile iliyo bora, isiyopinda ilionekana katika kila jaribio. Bwana alikuwa naye, na neno lake Bwana lilikuwa ndiyo sheria yake Yusufu.Mar 83.3

    Wale wanaojifunza Biblia, wanaoshika shauri la Mungu, na kumtegemea Kristo watawezeshwa kutenda kwa hekima nyakati zote na katika mazingira yote. Kanuni njema zitaelelezwa katika maisha halisi. Hebu ruhusu tu ukweli wa wakati huu upokelewe kwa upendo na uwe msingi wa tabia, na utazaa kusudi lisilobadilika, ambalo mivuto ya anasa, mabadiliko ya tamaduni, dharau itokanayo na upenzi wa dunia, na hata kelele za moyo wa mhusika mwenyewe za kutaka kuendekeza mapenzi ya nafsi havitaweza kuIibadili. Sharti kwanza dhamira ielimishwe, nia lazima itawaliwe. Kupenda kweli na haki lazima kutawale ndani ya roho, na tabia itaonekana ambayo mbingu yaweza kuithibitisha.Mar 83.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents