Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sabato Yatangazwa Kikamilifu Zaidi, Sura ya 162

  “Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” Ufunuo 14:6, 7.Mar 170.1

  Mwanzoni mwa wakati wa taabu, tulijazwa kwa Roho Mtakatifu kadiri tulivyopita huku na huko tukitangaza Sabato katika ukamilifu wake.Mar 170.2

  “Mwanzo wa wakati wa taabu,” uliotajwa hapa, hausondi kidole wakati mapigo yatakapomwagwa, ila kwa kipindi kifupi kabla hayajamwagwa, wakati Kristo akingali bado ndani ya patakatifu. Wakati huo, ambapo kazi ya wokovu inafikia hitimisho lake, kipindi cha taabu kitaijilia dunia, na mataifa yataghadhabika, ila yatazuiliwa yasije yakazuia kazi ya malaika wa tatu. Wakati huo “mvua ya masika,” au burudisho kutoka machoni mwa Bwana, Iitakuja, kutoa nguvu kwa sauti kuu ya malaika wa tatu, na kuwaandaa watakatifu kusimama katika kipindi ambapo mapigo saba ya mwisho yatamwagwa.Mar 170.3

  [Malaika wa Ufunuo 14] anatoa ujumbe ambao utatangazwa kwa ulimwengu muda mfupi kabla ya Kristo kurudi mawinguni. . . . Punde kabla ya kipindi hiki, ndipo, usikivu wa watu utaelekezwa kwa sheria ya Mungu iliyokanyagwa chini, ambayo imo katika sanduku la agano. . .Mar 170.4

  Wanagundua kuwa badala ya kushika Sabato ya siku ya saba, siku ambayo Mungu aliitakasa, na kuamuru iadhimishwe kama Sabato, wanatunza siku ya kwanza ya juma. lla ni shauku yao kuu kuyatenda mapenzi ya Mungu, nao wanaanza kuyachunguza Maandiko kujua sababu za mabadiliko hayo. Wakiwa wameshindwa kupata andiko lo lote linalohalalisha desturi hiyo, swali linaibuka, Je tuupokee ukweli huu usiopendwa na wengi, tutii amri za Mungu, ama tuendelee na ulimwengu, na kuyatii maagizo ya wanadamu? Wakiwa na Biblia zilizo wazi wanaomboleza, na kuomba, wakilinganisha andiko kwa andiko, hadi, wakishawishika na ile kweli, kwa dhamiri safi wanaamua kusimama upande wa washikao amri za Mungu.Mar 170.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents