Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sasa - Daima Sasa, Sura ya 47

    Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa. Mathayo 25:13.Mar 55.1

    Kuja kwa Kristo kutakuwa kama ambavyo ingelikuwa usiku wa manane, wakati wote wakiwa wamelala. Itakuwa vema kwa wote kuandaa hesabu zao kikamilifu kabla ya jua kutua. Matendo yote yapaswa kuwa sahihi, biashara zote zapaswa kuwa za haki, kati ya mtu na mwenzake. Hali zote za kutokuwa waaminifu, mazoea yote ya dhambi yapaswa kutupiliwa mbali. Mafuta ya neema yapaswa kuwa katika vyombo vyetu pamoja na taa zetu. . . Kwa hakika itakuwa huzuni kwa yule ambaye hali ya roho yake imekuwa na mfano tu wa utauwa huku akizikataa nguvu zake; ambaye amekuwa akimuita Kristo Bwana, Bwana, na bado hana mfano wake wala maandiko yake. ..Mar 55.2

    Kwa neema Mungu anatoa siku ya rehema, muda kwa ajili ya jaribio na maonjo. Anatoa mwaliko: “Mtafuteni Bwana maadam anapatikana, mwiteni maana yu karibu”. . .Mar 55.3

    Leo sauti ya rehema inaita, na Yesu anavuta watu kwa kamba za upendo; lakini siku yaja ambapo Yesu atavaa mavazi ya kisasi. . . Uovu wa dunia linaongezeka kila siku, na hatua fulani inapokuwa imefikiwa, kitabu kitakuwa kimefungwa, na hesabu zitakuwa zimekamilishwa. Hakutakuwa na kafara kwa ajili ya dhambi tena. Bwana anakuja. Kwa muda mrefu rehema imenyoosha mkono wa upendo, subira na uvumilivu, kuelekea kwa dunia yenye hatia. Mwaliko umetolewa, “Hebu na ashikilie nguvu zangu...” Lakini watu wametumia vibaya rehema na kukataa neema.Mar 55.4

    Kwa nini Bwana amekawiza ujio wake hivyo? Jeshi zima la mbinguni linasubiri kukamilisha kazi ya mwisho kwa dunia hii iliyopotea, na wakati huo huo kazi ikingoja. Ni kwa sababu wachache wanaodai kuwa na mafuta ya neema katika vyombo vyao na taa zao, hawajakuwa nuru ing’aayo na kuiangaza dunia. Ni kwa sababu wamishenari ni wachache. . .Mar 55.5

    Kila juma linapopita linamaanisha juma moja limepungua, kila siku ipitayo inaashiria siku moja ya karibu zaidi kufikia wakati uliowekwa kwa ajili ya hukumu. Inasikitisha kwamba wengi wanayo dini ya msimu - dini inayotegemea hisia na kutawaliwa na misisimko. “Yeye atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka.” Hivyo jichunguzeni na kuhakikisha kama mnayo mafuta ya neema ndani ya mioyo yenu. Kuwa na mafuta haya kutatengeneza ule utofauti utakaohitajika katika hukumu.Mar 55.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents