Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Usafi Moyoni na Maishani, Sura ya 80

  Heri wenye moyo safi; maana hao watamwona Mungu. Mathayo 5:8Mar 88.1

  Jijini mwa Mungu hapataingia chochote chenye kunajisi. Wote watakaofaa kuishi pale watakuwa wale ambao hapa wamekuwa safi mioyoni mwao. Kwake yeye anayejifunza kuhusu Yesu, kutadhihirika kutopenda tabia za uzembe, lugha isiyofaa, na mawazo yasiyo safi. Kristo anapokaa moyoni, kutakuwa na usafi na ustaarabu wa mawazo na tabia.Mar 88.2

  Lakini maneno ya Yesu.. .yana maana nzito zaidi - siyo safi tu kutokana na jinsi ulimwengu unavyouelewa usafi, yasiyo na chochote kilicho cha anasa, safi kwa kutokuwa na tamaa, lakini ya kweli hata katika mambo yaliyojificha na makusudi ya roho, yasiyo na kiburi wala kujitafutia mambo yake yenyewe, yasiyo na ubinafsi, yaliyo kama ya mtoto.Mar 88.3

  Vinavyofanana hutambuana. Huwezi kumjua Mungu kama hujakubali maishani mwako kanuni ya upendo wa kujinyima, ambayo ndiyo kanuni ya tabia yake. . .Mar 88.4

  Hapo Kristo atakapokuja katika utukufu wake, waovu hawataweza kudiriki kumtazama Yeye. Nuru ya uwepo wake, ambayo ni uhai kwa wale wampendao, ni mauti kwa wasio watauwa. . . Atakapotokea, wataomba wafichwe mbali na uso wake Yeye aliyekufa ili kuwakomboa.Mar 88.5

  Lakini kwa mioyo ya wale ambao watakuwa Wametakaswa kupitia kwa uwepo wa Roho Mtakatifu, yote yatakuwa yamebadilika. Hawa wanaweza kumjua Mungu. Musa alifichwa katika ufa wa mwamba wakati utukufu wa Bwana ulipofunuliwa kwake; na ndivyo ilivyo kwamba tunapofichwa katika Kristo ndipo tuwezapo kuuona upendo wa Mungu. . .Mar 88.6

  Kwa imani tunamuona hapa na sasa. Katika uzoefu wetu wa kila siku tunauona wema wake na huruma zake zinavyoonekana katika utoaji wake. Tunamtambua Yeye katika tabia ya Mwana wake. . .Walio wasafi wa moyo wanamuona Mungu katika uhusiano mpya na unaopendeza, kama Mkombozi wao; na kadiri waendeleapo kuangalia usafi na tabia yake inavyopendeza, wanatamani kuakisi sura yake. Wanamuona Yeye kama Baba anayetamani kukumbatia mwanae anayetubu, na mioyo yao inajazwa na furaha isiyoelezeka na utukufu kamili. . .Mar 88.7

  Walio safi katika roho wanaishi kama walio katika mwonekano dhahiri katika kipindi wapewacho hapa duniani. Vilevile, watamuona Yeye uso kwa uso hapo mbeleni, wakiwa katika hali ya kutokufa, kama alivyofanya Adamu alipotembea na kuongea na Mungu ndani ya Edeni.Mar 88.8

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents