Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mbingu Inakungoja, Sura ya 120

  Kama vile Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. Yohana 20:21.Mar 128.1

  Imeandikwa hivi kuhusu mitume, “Nao wale wakatoka, Wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo. Mk. 16:20. Kama vile Kristo alivyowatuma wanafunzi wake, vivyo hivyo anawatuma washiriki wa kanisa lake leo. Uwezo ule ule ambao mitume walikuwa nao upo kwa ajili yao. Washiriki wa sasa wanapaswa watambue kuwa kazi wanayoifanya ni ile ambayo Bwana ameitia muhuri. Mungu alimwambia Yeremia, “Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru. Usiogope kwa sababu ya hao; maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe.” Kisha Bwana akanyosha mkono wake na kukigusa kinywa cha mtumishi wake akisema, “Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako.” Yer. 1:7-9. Na sisi anatutuma twende kusema maneno aliyotupatia, huku tukihisi mguso wake mtakatifu katika vinywa vyetu.Mar 128.2

  Kristo amelipatia kanisa agizo takatifu. Kila mshiriki anapaswa kuwa njia ambayo Mungu anaweza kuitumia kuueleza ulimwengu juu ya hazina ya neema yake, yaani utajiri wa Kristo usiopimika. Hakuna kitu ambacho Mwokozi anakitamani kama kuona mawakala watakaowakilisha tabia yake kwa ulimwengu. Hakuna kitu ambacho ulimwengu unahitaji kama udhihirisho wa upendo wa Mwokozi kwa njia ya wanadamu. Mbingu yote masubiri watu ambao Mungu anaweza kuwatumia kuonesha nguvu ya Ukristo.Mar 128.3

  Kanisa ni wakala wa Mungu kwa ajili ya kutangaza ukweli, lina wezeshwa naye kufanya kazi maalum; na kama likiwa na uaminifu kwake, likitii amri zake zote, ndani yake kutakaa ukamilifu wa neema ya Mungu. Kama Iitasimama katika utii wake, kama litamheshimu Mungu wa Israel, hakuna nguvu inayoweza kulipinga.Mar 128.4

  Juhudi kwa ajili ya Mungu na kazi yake iliwafanya wanafunzi kushuhudia Injili kwa nguvu kubwa. Je, haipaswi nguvu kama hiyo kuamsha mioyo yetu kwa azma ya kusimulia kisa cha upendo unaokomboa, kisa cha Kristo aliyesulubiwa? Fursa aliyopewa kila Mkristo siyo kutazamia ujio wa Mwokozi, bali pia kuuharakisha.Mar 128.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents