Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Nafuu Toka Maumivu ya Mwili, Sura ya 177

    Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. Mathayo 10:7, 8.Mar 185.1

    Nyakati za hatari ziko mbele yetu. Dunia nzima itahusika na fadhaa na dhiki, maradhi ya kila namna yatakuwa katika jamii ya watu, na kutojua kanuni za afya kunakotawala sasa kutatoa matokeo ya mateso makubwa na vifo vingi vya watu ambao wangeweza kuokolewa...Mar 185.2

    Ushari wa kidini unapoendelea kuondoa uhuru katika taifa letu, wale ambao wangesimamia uhuru wa dhamiri watawekwa katika mazingira yasiyo mazuri. Kwa faida yao wenyewe, wanapaswa kutumia akili zao kujua mambo ya magonjwa, vyanzo vyake, namna ya kuyazuia, na jinsi ya kutibu. Wale wanaofanya hivi watapata nafasi ya kufanya kazi popote. Watakuwapo wanaotaabika, wengi sana, ambao watahitaji msaada, wala siyo tu kati ya wale wa imani yetu, bali kwa wingi toka kwa wale wasioujua ukweli. Kazi ya tiba ikifanyika pamoja na utoaji wa ujumbe wa malaika watatu, italeta matokeo ya ajabu. Inapaswa kuwa kazi inayotakasa, inayounganisha, ikipelekana na ile kazi ambayo yule Mkuu wa kanisa alituma wanafunzi wake wa kwanza kuifanya.Mar 185.3

    Alipokuwa anawaita wanafunzi wake pamoja, Kristo aliwapa utume wao. . . . “Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.” “Angalieni mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.” Mt. 10:7,8, 16.Mar 185.4

    Ni vema kwetu kusoma sura hii na turuhusu maelekezo yake yatuandae kwa ajili ya kazi zetu. Wanafunzi wa awali walikuwa wakienda kutumika katika majukumu ya Kristo, chini ya utume wake. Roho wake aliandaa njia mbele yao. Walipaswa wahisi ya kwamba wakiwa na ujumbe wa kuutoa wa namna hiyo, baraka za namna hiyo za kutoa, walikuwa wapokelewe majumbani mwa watu.Mar 185.5

    Mungu anagusa mioyo kupitia katika kutuliza maumivu ya kimwili. Mbegu ya kweli yaweza kudondoshwa mawazoni mwa mtu, na kisha Mungu akaimwagilia. Yawezekana subira ikahitajika sana kabla ya mbegu kuonesha dalili za uhai, lakini hatimaye itachipua na kuota, na baada ya kukua itazaa matunda ya uzima wa milele.Mar 185.6

    Wanadamu ni wazito sana katika kuelewa maandalizi ya Mungu anayoyafanya kwa ajili ya siku ya uweza wake!Mar 185.7

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents