Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Hekima Wanayoihitaji Washika Sabato, Sura ya 169

  Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua. Mathayo 10:16.Mar 177.1

  Wakati mazoea ya watu hayagongani na sheria ya Mungu, mwaweza kukubaliana nayo. Kama wafanyakazi watashindwa kulifanya hili, siyo tu kwamba watazuia kazi yao wenyewe, bali pia watakuwa wameweka vikwazo katika njia ya wale ambao wanawafanyia kazi, na kuwazuia wasiipokee kweli. Wamishenari watakuwa na fursa bora sana siku ya Jumapili kwa ajili ya kuendesha shule za Jumapili, na kuwafikia watu katika namna iliyo sahili kadiri iwezekanavyo, huku wakiwaambia juu ya upendo wa Yesu kwa wadhambi, na kuwaelimisha katika Maandiko...Mar 177.2

  Kwa sasa, ushikaji wa Jumapili siyo jaribu. Wakati utakuja, ambao siyo tu kwamba watu watapiga marufuku kufanya kazi siku ya Jumapili, lakini pia watajaribu kuwalazimisha watu kufanya kazi siku ya Sabato, na badala yake waikubali Jumapili ama sivyo waache uhuru na maisha yao. Lakini wakati kwa ajili ya hilo haujafika bado, kwani kweli sharti iwasilishwe kwa ukamilifu kabisa mbele za watu kama ushuhuda. . . .Mar 177.3

  Nuru niliyonayo ni hii, watumishi wa Mungu wanapaswa kwenda kimya kimya kazini, wakihubiri kweli kuu za thamani za Biblia - Kristo, Yeye aliyesulubiwa. Upendo wake na kafara yake isiyo na mwisho wakionesha kuwa sababu ya kufa kwa Kristo ni kwamba sheria ya Mungu haibadiliki na ya milele. Sabato inapaswa ifundishwe kwa namna iliyo thabiti, lakini uwe mwangalifu jinsi unavyoshughulikia sanamu iitwayo Jumapili. Neno moja kwa mwenye hekima linatosha. . .Mar 177.4

  Kuacha kufanya kazi siku ya Jumapili siyo kupokea alama ya mnyama; na pale ambapo kufanya hivyo (kutofanya kazi) kutasaidia katika kuiendeleza kazi, na iwe hivyo. Hatupaswi kulazimika kufanya kazi siku ya Jumapili. . . .Mar 177.5

  Wakati wale wanaosikia na kuona nuru ya Sabato wanapochukua hatua ya kuikubali kweli na kushika siku takatifu ya Mungu, mambo magumu yataibuka; kwani juhudi zitatumika ili kuwalemea na kuwashurutisha wanaume kwa wanawake kuasi sheria ya Mungu. Hapa wanapaswa wasimame imara, ili wasiivunje amri ya Mungu; na kama upinzani na mateso yataendelezwa kwa makusudi, hebu na wasikie maneno ya Kristo: “lakini watakapowafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine.”Mar 177.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents