Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kutafakuri kwa Hali ya Juu Kuliko Zote,Sura ya 69

    Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baha, kwamba tuitwe wana wa Mungu. 1 Yohana 3:1.Mar 77.1

    Ni upendo wa ajabu, upendo usio kifani, ambapo wadhambi na wageni kama tulivyo, tunaweza kurejeshwa kwa Mungu na kupangwa kuwa watoto kama sehemu ya familia! Tunaweza kumuita kwa jina lile tamu, “Baba yetu.” . . .Mar 77.2

    Upendo wote wa Baba ambao umeshuka toka kizazi hadi kizazi kupitia katika mfereji wa mioyo ya watu, chemchemi zote za wema ambazo zimefunguka katika roho za watu, zipo kama kijito kidogo tu dhidi ya bahari isiyo na mwisho unapolinganisha na upendo usio na mwisho wa Mungu. Ulimi hauwezi kuutamka; kalamu haiwezi kuuchora. Waweza kuutafakari kila siku ya maisha yako; unaweza kuyachunguza Maandiko kwa makini ili upate kuyaelewa; waweza kuitisha kila aina ya nguvu na uwezo ambao Mungu amekupatia, katika jitihada ya kuelewa upendo na rehema ya Baba wa mbinguni; na bado utakuwa na umilele mbele. Unaweza kujifunza upendo huo kwa karne nyingi lakini kamwe huwezi kuelewa kikamilifu marefu, mapana, kina na urefu wa upendo wa Mungu katika kumtoa Mwanae ili aufie ulimwengu. Umilele wenyewe hauwezi kuufunua kikamilifu. Hata hivyo, tunapoendelea kujifunza Biblia na kutafakari maisha ya Kristo na mpango wake wa ukombozi, mada hizi kuu zitafunguka katika fahamu zetu zadi na zaidi.Mar 77.3

    Kristo alikuja kumfunua Mungu kwa ulimwengu kama Mungu wa upendo, aliyejaa huruma, wema, na rehema.Mar 77.4

    Ni vema kutumia saa moja ya tafakuri kila siku katika kupitia maisha ya Kristo tokea horini hadi Kalvari. Tunapaswa kuyaangalia hatua kwa hatua na kuruhusu mawazo yetu yanase kikamilifu kila tukio, hususani yale ya kufungia huduma yake hapa duniani. Kwa kutafakari mafundisho na mateso yake hivyo, na kafara isiyo na mwisho iliyotolewa na Yeye kwa ajili ya ukombozi wa watu, tunaweza kuimarisha imani yetu, kuamsha upendo wetu, na kujazwa ndani kabisa ndani yetu na roho yule aliyemtegemeza Mwokozi wetu. Kama kweli tunataka kuokolewa hapo mwisho sharti tujifunze somo la kujutia dhambi na imani chini ya msalaba.... Kila namna ya uadilifu na ukarimu ulio ndani ya mwanadamu utainuka pale tafakuri ya Kristo msalabani inapopata nafasi.Mar 77.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents