Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kiwango cha Juu, Sura ya 33

  Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi BWANA ni mtakatifu, nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu. Mambo ya Walawi 20:26.Mar 41.1

  Niliona pia ya kuwa wengi hawatambui wawe jinsi gani ili waishi mbele za Bwana bila kuhani mkuu katika hekalu wakati wa taabu. Wale wanaopokea muhuri wa Mungu aliye hai na hivyo kulindwa wakati wa taabu sharti waakisi mfano wa Yesu kikamilifu.Mar 41.2

  Niliona kuwa wengi wanadharau maandalizi yanayohitajika sana na wanatazamia wakati wa “kuburudishwa” na “mvua ya masika” ili iwafanye wastahili kusimama katika siku ile ya Bwana na kuishi mbele zake. Niliona wengi sana wakati wa taabu wakiwa bila kinga! Walikuwa wamedharau maandalizi yaliyohitajika; kwa hiyo hawangeweza kupokea burudiko ambalo wote wanapaswa kuwa nalo ili wastahili kuishi mbele za Mungu mtakatifu. Wale wanaoshindwa kusafisha roho zao kwa kuutii ukweli wote watafikia wakati wa mapigo yatakaposhushwa, na ndipo watakapoona kuwa walihitaji kuchongwa na kuwekwa sawa kwa ajili ya kuwa sehemu ya jengo. Lakini hakutakuwa na Mpatanishi kwa ajili ya kuwaombea mbele za Baba. Kabla ya wakati huu, lile tamko zito sana litakuwa limeshatolewa, “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu: na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.”Mar 41.3

  Niliona ya kuwa hakuna mtu ambaye angepata “kuburudishwa” kama hajapokea ushindi dhidi ya kila kinachomzonga, kiburi, ubinafsi, kupenda dunia, na kila neno na tendo lisilo sahihi. Kwa hiyo, tunapaswa basi kusogea karibu na Bwana zaidi na zaidi na tutafute kwa dhati maandalizi yaliyo muhimu ili tuweze kusimama katika pambano katika siku ya Bwana. Hebu wote na wakumbuke ya kwamba Mungu ni mtakatifu na kwamba hakuna awezaye kuwa katika uwepo wake isipokuwa walio watakatifu.Mar 41.4

  Leo tunapaswa kuangalia kuwa hatujikwai kwa neno au tendo....Sharti tumtafute Mungu leo na tuazimu ya kwamba hatutajituliza kwa kuridhika bila ya uwepo wake. Tunapaswa tukeshe na kufanya kazi na kuomba kana kwamba siku hii ndiyo ya mwisho tuliyopewa. Maisha yetu basi, yanapaswa kuwa yenye bidii ya juu sana. Tunapaswa kumfuata Yesu kwa karibu sana kwa maneno na matendo yetu yote.Mar 41.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents