Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Machafuko ya Sauti Nyingi, Sura ya 181

  Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Ufunuo 18:4.Mar 189.1

  Kazi ya mwisho ya kuuonya ulimwengu inadhihirisha miito miwili inayotolewa kwa makanisa. Ujumbe wa malaika wa pili ni, “Umeanguka umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.” Vilevile katika kilio kikuu cha yule malaika wa tatu sauti inasikika kutoka mbinguni ikisema, “Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.”Mar 189.2

  Kama jinsi Mungu alivyowaita wana wa Israeli kutoka Misri, ili wapate kuishika Sabato, vivyo hivyo anawaita watu wake watoke Babeli, ili wasimwabudu mnyama na sanamu yake...Mar 189.3

  Baada ya ukweli kuhubiriwa kama ushuhuda kwa mataifa yote, kila namna ya nguvu ya uovu itatenda kazi, na mawazo yatachanganywa na sauti nyingi zikilia, “Tazama Kristo yuko hapa, tazama yuko pale. Huu ndio ukweli, ninao ujumbe toka kwa Mungu, amenituma na nuru kuu.” Ndipo kutakuwa na kuondolewa kwa mipaka na jaribio la kuvunja mihimili ya imani yetu. Kutakuwa na jitihada ya makusudi ya kutukuza sabato ya uongo na kumdharau Mungu mwenyewe kwa kubadili siku aliyoibariki na kuitakasa. Sabato hii ya uongo itashinikizwa na sheria ya ukandamizaji... Lakini ingawa Shetani anatenda kazi kwa kutumia maajabu yake yadanganyayo, wakati uliotajwa kwenye Ufunuo litatimizwa, na yule malaika mkuu ambaye ataing’aza dunia kwa utukufu wake, atatangaza kuanguka kwa Babeli, na kuwaita watu wa Mungu waiache Babeli.Mar 189.4

  Ni Iini dhambi zake zitafika hadi mbinguni? Wakati sheria ya Mungu itakapobatilishwa kwa sheria ya kiserikaIi. Hapo ukomo wa watu wa Mungu utakuwa ni fursa kwake kuonesha nani aliye Mtawala wa mbingu na dunia. Mamlaka ya Shetani inapotibua mambo kutoka chini, Mungu atatuma nuru na uweza kwa watu wake, ili kwamba ujumbe wa kweli utangazwe duniani kote.Mar 189.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents