Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Lulu ya Mbinguni Isiyo na Kasoro, Sura ya 64

    Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri; naye alipoona lulu ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua. Mathayo 13: 45,46.Mar 72.1

    Kristo mwenyewe ni lulu ya thamani kuu...Haki ya Kristo, haina dosari wala waa kama ilivyo lulu iliyo nyeupe na safi. Hakuna mtu awezaye kufanya karama ya Mungu iliyo kuu kuwa bora kuliko jinsi ilivyo. Haina kasoro. Ndani yake Kristo, “hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.” Kol. 2:3. Yeye amefanywa kwetu kuwa “hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi.” 1 Kor. 1:30. Yote yawezayo kukidhi mahitaji na shauku ya roho ya mtu, kwa ajili ya ulimwengu huu na ule ujao, hupatikana katika Kristo. Mkombozi wetu ni lulu ya thamani kubwa sana ambayo kwa kulinganisha na vitu vingine, vyote kando ya yeye ni hasara. . .Mar 72.2

    Katika mfano uliotajwa katika Biblia, lulu siyo zawadi. Mfanyabiashara aliinunua kwa gharama ya kuuza vyote alivyokuwa navyo. Wengi wanahoji juu ya hili kwa sababu Kristo anawakiIishwa katika Maandiko kama zawadi. Ndiyo, Yeye ni zawadi, lakini ni kwa wale tu wajitoao nafsi zao, roho zao, miili yao na mioyo yao kwake yeye bila kuacha chochote. Tunapaswa kujitoa kwa Kristo, kuishi maisha ya utii wa dhati kwa matakwa yake yote. Vyote tulivyo navyo, vyote vitufanyavyo kuwa jinsi tulivyo ni vya Bwana, na vyapaswa kuwekwa wakfu kwa utumishi wake. Tujinapojitoa kwake kwa ukamilifu hivyo, Kristo hujitoa kwetu pamoja na hazina zote za mbinguni. Tunapata lulu ya thamani kuu. . .Mar 72.3

    Katika soko ambapo rehema ya kimbingu inatawala, lulu ya thamani inawakilishwa kama inayonunuliwa bila fedha na bila thamani. Katika soko hili wote wanaweza kupata bidhaa za mbinguni. Hazina ya vito vya kweli inafunguliwa kwa ajili ya wote. . . Sauti ya Mwokozi kwa udhati kabisa inatualika kwa upendo: “Nakupa shauri ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri”. . .Walio maskini sana wanao uwezo kama walio matajiri sana kupata wokovu: kwani hakuna kiasi cha utajiri wa dunia kiwezacho kuipata hazina hii. Hii hupatikana kwa utiii, kwa kujitoa kwa Kristo kama mali aliyoinunua mwenyewe. . .Mar 72.4

    Hatuwezi kuununua wokovu, bali twapaswa kuutafuta kwa shauku na subira kama watu waachao kila kitu katika dunia ili kuupata.Mar 72.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents