Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Nyakati na Majira, Sura ya 128

    Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba . aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe. Matendo 1:7.Mar 136.1

    Mungu ameweka katika uwezo wake nyakati na majira . Je, kwa nini Mungu hajatupatia ujuzi huu? Kwa sababu tusingeweza kuutumia vema kama tungekuwa nao. Kutokana na ujuzi huu ingetokea hali ya mambo kati ya watu ambayo ingedhoofisha kazi ya Mungu kwa kiasi kikubwa katika kuandaa watu wawe tayari kusimama katika siku ile kuu inayokuja... Yesu aliwaambia wanafunzi wake “wakeshe,” lakini hakuwapa muda kamili. Wafuasi wake wanapaswa kuwa katika mahali kama pa wale wanaosikiliza maelekezo ya Nahodha wao; wanapaswa wakeshe, wangoje, waombe, na kufanya kazi, kadiri wanavyokaribia wakati wa kuja kwa Bwana; lakini hakuna anayeweza kutabiri wakati utafika lini; kwa sababu “habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye.” Huhitaji kusema kuwa atakuja katika mwaka mmoja, miwili, au mitano ijayo, na wala hupaswi kuahirisha kuja kwake kwa kusema kwamba hatatokea katika miaka kumi au ishirini ijayo... Si nafasi yetu sasa kujua wakati halisi wa ama kumwagwa kwa Roho Mtakatifu au kuja kwa Kristo.Mar 136.2

    Nilielekezwa kuwaangalia wale walio katika makosa makubwa ya kuamini kwamba ni wajibu wao kwenda kwenye lile jiji la Yerusalemu ya zamani, | imeandikwa mapema miaka ya 1850 wakati wale walioeneza mafundisho juu ya “kipindi kinachokuja” walipofundisha kuwa yerusalemu ya zamani itajengwa kama kituo kwa ajili ya ushuhuda wa kikristo ili kutimiza unabii fulani wa agano la kale.| na wakidhani kuwa wana kazi ya kufanya pale kabla Bwana hajaja. Mtazamo huo unalenga katika kuteka mawazo na shauku ya watu kutoka katika kazi ya Bwana iliyopo sasa, chini ya ujumbe wa yule malaika wa tatu; kwani wale wanaofikiri kwamba sharti waende Yerusalemu watakuwa wameweka mawazo yao pale, na raslimali walizonazo zitazuiwa toka katika kuunga mkono kazi ya kuupeleka ukweli wa leo, ili wao waweze kwenda pale. Niliona ya kuwa utume wa namna hiyo usingezaa chochote chema, kwamba ingechukuwa muda mrefu sana kuwafanya Wayahudi wachache waamini hata tu kuja kwa Kristo mara ya kwanza, licha ya kuamini ukweli zaidi juu ya kuja kwake mara ya pili.Mar 136.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents