Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Lindo la Mwisho, Sura ya 48

  Kesheni basi kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi; asije akawasili ghafla akawakuta mmelala. Marko 13:35, 36.Mar 56.1

  Kundi liliwekwa mbele yangu... Macho yao yalikuwa yameelekezwa mbinguni, na maneno ya Bwana wao yalikuwa midomoni mwao: “Niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni”. . . Kabla hakujapambazuka alfajiri Bwana anaruhusu mwonekano wa kuchelewa. Lakini hataki lile kundi liruhusu uchovu, wala uzembe katika kukesha, kwa sababu tu asubuhi haiwafikii katika wakati waliotarajia...Mar 56.2

  Niliona ya kwamba haingewezekana kuwa na mapenzi na shauku katika kufungamana na mambo ya ulimwengu huu, kujilimbikizia vitu vya kidunia, wakati huo huo mtu akiwa katika hali ya kusubiri na kukesha kama Mwokozi alivyoamuru. Malaika akasema, “Wanaweza kukamata ulimwengu wa aina moja tu. Ili kupata hazina za mbinguni, sharti waachilie mali za kidunia. Hawawezi kuwa na pande zote.”. . .Mar 56.3

  Niliona ya kwamba lindo baada ya lingine lilikuwa likipita. Kwa sababu ya hali hii, je, ni sawa kutokuwa na hadhari? La hasha! Kuna umuhimu mkubwa zaidi wa kukesha kusikokoma, kwani sasa nafasi ni ndogo kuliko ilivyokuwa wakati wa lindo la kwanza...Kama tulikesha kwa hadhari sana wakati ule, je hatuknhitajika kukesha maradufu zaidi katika lindo la pili? Kupita kwa lindo la pili kulitufikisha katika lindo la tatu, na sasa hatuna udhuru kabisa kuzembea katika kukesha kwetu. Lindo la tatu linatualika katika umuhimu mara tatu. Usiku mrefu wa giza ni jaribio zito; lakini asubuhi inacheleweshwa kwa sababu ya rehema, kwani kama Bwana angekuja, wengi wangekutwa wakiwa hawajawa tayari. Kwa sababu Mungu hapendi watu wake waangamie ndiyo sababu ya uchelewaji huu.Mar 56.4

  Tofauti kati ya wale waipendao dunia na wale wampendao Kristo iko wazi kiasi ambacho mtu hawezi kuchanganya makundi haya mawili. Wakati wale waipendao dunia bidii yao yote na shauku yao ipo katika kukusanya hazina ya dunia, watu wa Mungu hawaambatani na dunia, bali huonesha kwa bidii yao katika kukesha, hali ya subira waliyonayo, ya kwamba wamebadilishwa, kwamba duniani siyo nyumbani kwao, kwani wanatafuta nchi iliyo bora zaidi, ya mbinguni.Mar 56.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents