Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uponyaji wa Roho Zenye Ugonjwa wa Dhambi, Sura ya 61

  Kichwa chote ni kigonjwa, moyo wote umezimia. Tangu wayo wa mguu hata kichwani hamna uzima ndani yake; bali jeraha na machubuko na vidonda vitokavyo usaha; havikufungwa, havikuzongwa- zongwa, wala havikulainishwa kwa mafuta. Isaya 1:5,6.Mar 69.1

  Ipo dawa kwa ajili ya roho iliyo na ugonjwa wa dhambi. Dawa hiyo ni Yesu. Mwokozi ni wa thamani! Neema yake inatosha kwa ajili ya wadhaifu; na hata walio na nguvu wanapaswa kupokea neema yake la sivyo wataangamia. Niliona jinsi neema hii iwezavyo kupatikana. Ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiwa peke yako pale, msihi Mungu: “Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu.” Uwe umenia yale uyasemayo, sema kwa dhati. . . sala kama ya Yakobo, unapomlingana katika sala. Lazima uumie. . . unapaswa kuweka jitihada yako hapo katika sala...Mar 69.2

  Mtafute Bwana kwa moyo wako wote. Njoo ukiwa na ari, na pale unapohisi ya kwamba bila msaada wake utaangamia, unapokuwa na shauku juu yake kama ayala alivyo akitamani maji katika kijito, ndipo Bwana atakupa nguvu upesi. Hapo ndipo utakuwa na amani ipitayo maelezo. Kama unategemea wokovu, sharti uombe. Jipe muda wa kutosha. Usiwe na papara na uzembe katika sala zako. Msihi Mungu akupe matengenezo ya kina, ili tunda la Roho lionekane ndani yako, na kisha ung’ae kama nuru duniani. Usiwe kizuizi au laana kwa mpango wa Mungu; waweza kuwa msaada, mbaraka. Je, Shetani anakwambia ya kwamba waweza kufurahia wokovu kamili bila chochote? Usimuamini.Mar 69.3

  Niliona ya kwamba ni nafasi nzuri na ya upendeleo kwa kila Mkristo kufurahia kazi za ndani kabisa za Roho wa Mungu. Amani ya ndani, iliyo nzuri ya kimbingu itatawala mawazo, na utapenda kumtafakari Mungu na mbingu. Utajisherehesha na ahadi zenye utukufu za neno lake. . .Mar 69.4

  Kama wale wajiitao Wakristo watampenda Yesu kuliko dunia, watapenda kuzungumza juu yake, aliye rafiki bora kuliko wote kwao, ambaye kwake wameweka mapenzi yao ya juu zaidi. Alikuja kuwaokoa pale walipohisi wamo katika hali ya kupotea na kuangamia. Walipokuwa wamechoka na kulemewa na dhambi, walimgeukia. Aliondoa mzigo wao wa hatia na dhambi. . . kisha akabadili kabisa mkondo wa mapenzi yao. Mambo yale ambayo walipata kuyapenda, sasa wanayachukia; na yale waliyoyachukia, sasa wanayapenda. Je, badiliko hili limetokea ndani yako?Mar 69.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents