Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mungu Anapojaza Palipopungua, Sura ya 107

  Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. 2 Wakorintho 6:1.Mar 115.1

  Tunapaswa kuwa watendakazi wenza katika kazi ya Mungu duniani kote: popote palipo na roho zinazohitaji wokovu, tunapaswa kutoa msaada, ili wana na mabinti waletwe kwa Mungu. Mwisho umekaribia, na kwa sababu hiyo tunapaswa kutumia kwa hekima kila uwezo tuliopewa na kila nyenzo ambayo itatusaidia katika kazi...Mar 115.2

  Lazima malaika wanahisi vibaya sana waonapo ya kuwa ule mwisho umekaribia, na wale ambao wamekabidhiwa ujumbe wa mwisho wa rehema wamesongamana pamoja, wakihudhuria mikutano kwa ajili ya faida ya roho zao tu, huku wakihisi kutoridhika pale ambapo hakuna mahubiri kwa wingi na ya nguvu, hali hawaoni mzigo na hivyo kutofanya mengi kwa ajili ya wokovu wa wengine. Wote ambao wameungana na Kristo kwa imani iliyo hai watakuwa washirika wa asili ya kimbingu. Hawa watadumu kupokea toka kwake uhai wa kiroho, na hawatakaa kimya.Mar 115.3

  Daima maisha hujionesha katika matendo. Kama moyo upo hai, utatuma damu kwenda kwa kila sehemu ya mwili. Wale ambao mioyo yao imejazwa na uhai wa kiroho hawatahitaji kushawishiwa kuuonesha hadharani. Uhai wa kiroho utabubujika toka kwao katika mkondo mzito uliojaa neema. Wanaposali, wanaponena, na wanapotenda kazi, Mungu atatukuzwa...Mar 115.4

  Kazi itoayo matokeo yanayodumu sana tena yaliyo makuu siyo ya wale ambao ni werevu sana au wenye talanta sana. Watenda kazi stadi zaidi ni nani? Ni wale waitikiao wito: “Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo.”Mar 115.5

  Kama watu ambao Mungu amewatunukia talanta za ufahamu watakataa kuzitumia karama hizi kwa utukufu wake, baada ya kuwajaribu atawaachilia mbali kwa mawazo yao wenyewe na atachukua watu ambao hawaonekani kuwa na karama za ajabu kiasi kikubwa, wasiojiamini sana, na atachukua wanyonge na kuwatia nguvu kwa sababu wanamtegemea Mungu awatendee mambo yale ambayo hawawezi kujitendea. Mungu atakubali huduma itokanayo na mioyo iliyotolewa kikamilifu, na atajaza katika mapungufu yao.Mar 115.6

  Malaika wanasikiliza aina ya taarifa unayoitoa kwa ulimwengu kumhusu Bwana wako wa mbinguni.Mar 115.7

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents