Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uungwana wa Kujikana, Sura ya 112

  Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu. Gal. 2:20Mar 120.1

  Paulo aliipokea neema ya Kristo kwa imani, na neema hiyo ilimpatia mahitaji ya lazima ya nafsi yake. Aliipokea zawadi iliyotoka mbinguni kwa imani, na akaitoa kwa roho zilizokuwa na kiu ya nuru. Hivyo ndivyo tunavyopaswa kuwa. . . Omba ili uwe na imani hiyo. Amini kwamba Mungu atakupatia.Mar 120.2

  Kuna kazi kubwa inayohitajika kufanyika katika ulimwenguni wetu. Hii si ndoto. Mbele yetu upo ukweli ulio hai. Udhihirisho wa nguvu za Shetani utaonekana katika kila upande. Tunapaswa kushirikiana naye Yeye anayerejesha na kuinua. Na tusisahau kwamba yule anayemtumikia, Kristo anapaswa kupata nguvu yake kutoka katika chanzo cha nguvu zote.... Wakristo wanahitaji uwezo wa kufikiri, uthabiti wa nia, na ujuzi unaotokana na kusoma neno la Mungu. Hawapaswi kuzijaza akili zao kwa mambo yasiyokuwa na maana. Wanapaswa kufanywa upya kila siku katika uwezo wao wa kiroho.Mar 120.3

  Jifunze kwake Yeye aliyesema, “Mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo.” Ukijifunza kwake litapata pumziko. Siku kwa siku utakuwa anapata uzoefu wa mambo ya Mungu, siku kwa siku utakuwa unauona ukuu wa wokovu wake na utukufu wa kushikamana naye. Utakuwa anajifunza zaidi namna ya kuishi kama Kristo wakati wote na utakuwa unazidi kufanana na Mwokozi wakati wote.Mar 120.4

  Tukiifia nafsi, tukiikuza dhana ya vile Kristo anavyoweza kuwa kwetu, na vile tunavyoweza kuwa kwake, kama tukishikamana pamoja katika umoja wa jumuiya ya Kikristo, Mungu atatutumia kwa uwezo mkubwa. Hapo ndipo tutakapotakaswa na ile kweli. Tutakuwa tumeteuliwa kweli na Mungu na kuongozwa na Roho wake. Kila siku tunayoishi itakuwa na thamani kwetu, kwani ndani yake tutakuwa tunaona fursa ya kutumia karama tulizopewa kwa ajili ya kuwabariki wengine.Mar 120.5

  Tunapaswa kusahau nafsi na kuzania katika kuwahudumia wengine. . . Tunaweza tusikumbuke tendo fulani la ukarimu tunalolifanya,. . . lakini katika maisha ya milele kila tendo lililotendwa kwa ajili ya wokovu wa roho, kila neno lililonenwa kwa ajili ya kuwafariji watoto wa Mungu, Iitadhihirishwa kwa mng’ao wake wote; na matendo haya yaliyofanywa kwa ajili ya Kristo yatakuwa sehemu ya furaha yetu milele.Mar 120.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents