Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Karamu Inayoridhisha, Sura ya 38

  Heri wenye njaa na kiu ya haki; maana hao watashibishwa. Mathayo 5:6Mar 46.1

  Laiti wale walioridhika na hali yao ya kudumaa na kulemaa katika mambo ya kimbingu wangepelekwa mbinguni mara moja na kwa muda mfupi washuhudie hali ya utakatifu na ukamilifu wa juu inayodumu pale kila roho imejazwa na upendo; kila uso uking’aa kwa furaha;. . . nauliza kwamba je, watu hawa, wangeweza kujichanganya na kusanyiko la kimbingu, na kushiriki nyimbo zao, na kustahimili utukufu uliosafi wa juu, utokao kwa Mungu na Mwanakondoo? La hasha!. . .Mar 46.2

  Wale ambao wamezoeza mawazo yao kufurahia mambo ya kiroho ndio watakaobadilishwa na hivyo kutozidiwa na nguvu ya usafi upitao maelezo wa utukufu wa mbinguni. Waweza kuwa na ujuzi mwingi katika sanaa, waweza kuwa na ufahamu wa sayansi, waweza pia kuwa na uwezo wa juu katika muziki na uandishi, tabia yako yaweza kuwa imewapendeza wafanyakazi wenzako, lakini je, haya hukusadiaje katika maandalizi ya kwenda mbinguni? Haya yanakuandaaje kusimama mbele za mahakama ya Mungu?Mar 46.3

  Usidanganyike. Mungu hadhihakiwi. Ni utakatifu pekee ndiyo utakaokuandaa kwa ajili ya Mbinguni. Utauwa uliojaribiwa ulio wa kuaminika peke yake utakupatia tabia safi iliyotukuka na kukuwezesha kuingia mbele za Mungu, yeye aketiye katika utukufu usio wa kuchezea. Tabia ya kimbingu inapaswa kupatikana hapa duniani, la sivyo haitapatikana kabisa.Mar 46.4

  Kutamani wema na utakatifu wa kweli ni sahihi; lakini kama mtu akikomea hapo, tamaa hiyo haisaidii kitu. Ni sahihi kuwa na makusudio mazuri, lakini hayatazaa matunda yoyote kama hayataambatana na nia thabiti ya kuyatekeleza. Wengi watapotea hali wakitamani kuwa Wakristo; bali hawakuifanya juhudi za makusudi na hivyo watakapopimwa kwenye mizani wataonekana kupungua. Nia inapaswa iwekwe katika mwelekeo sahihi. Nitakuwa Mkristo aliyetoa moyo wote. Nitajua urefu, na upana, kimo na kina, cha upendo ulio mkamilifu.Mar 46.5

  Sikiliza maneno ya Yesu: “Heri wenye njaa na kiu ya haki; maana hao watashibishwa.” Mahitaji ya kutosha yaridhishayo roho iliyo na njaa na kiu ya haki yanatolewa na Kristo.Mar 46.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents