Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Nyakati za Taabu Ziko Mbele Yetu, Sura ya 167

  Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote. Ufunuo 7:1.Mar 175.1

  Malaika wanne wenye uwezo bado wanashikilia pepo nne za dunia. Uangamivu wa kutisha unazuiwa kuja kikamilifu. Pepo zitatibua mataifa na kuyapelekea katika pigano moja kubwa la kutisha, wakati malaika wanazishikilia pepo nne, wakizuia nguvu iliyo mbaya sana ya Shetani ili isitende kazi katika hasira yake hadi watumishi wa Mungu watakapotiwa muhuri katika vipaji vya nyuso zao.Mar 175.2

  Dalili za nyakati zinathibitisha kuwa hukumu za mbinguni zinamwagwa, kwamba siku ya Bwana imefika. Magazeti ya kila siku yamejaza dalili za pambano kali linalokuja siku zijazo. Ujasiri katika ujambazi unazidi kuonekana mara kwa mara. Migomo imekuwa ya kawaida. Wizi na mauaji vinafanyika kila upande. Watu ambao wamepagawa na pepo wanachukua maisha ya watu wazima na watoto. Mambo yote haya yanashuhudia kuwa kuja kwa Bwana kuko karibu.Mar 175.3

  Roho wa Mungu anayezuia anaondolewa sasa kutoka duniani. Vimbunga, tufani, dhoruba, maafa baharini na nchi kavu, vitafuatana kwa karibu sana na kwa upesi. Dalili ambazo zinaongezeka kutuzunguka, zikiarifu juu ya ujio unaokaribia wa Mwana wa Mungu, badala ya chanzo chake halisi kutambuliwa, inafikiriwa kuwa zinatokana na mambo mengine tu...Mar 175.4

  Wakati umetufikia ambapo kutakuwa na simanzi duniani kiasi ambacho hakuna dawa ya kibinadamu itakayoweza kuiondoa. Hata kabla ya kuja kwa maangamizo makuu ya mwisho duniani, sanamu za majivuno za ukuu wa watu zitaangushwa chini. Hukumu za Mungu zitashuka kuwaadhibu wale ambao wamedumu katika dhambi hali wakiwa na nuru kuu mbele yao. Majengo yanajengwa kwa gharama kubwa, ambayo yamekusudiwa kutoweza kuungua moto. Lakini kama jinsi Sodoma ilivyoteketea katika miali ya ghadhabu ya Mungu, vivyo hivyo majengo haya wanayojivunia yatakuwa majivu. Nimeshuhudia vyombo vya majini vilivyotengenezwa kwa fedha nyingi sana vikipambana na bahari iliyochafuka, viking’ang’ana katika kukabili mawimbi marefu. Lakini pamoja na hazina zao zote za dhahabu na fedha, na pia pamoja na mzigo wa watu ndani yake, vilizama ndani ya kaburi la maji.... Lakini hata kati ya mwamko wa ghasia, kukiwa na machafuko kila mahali, ipo kazi ya kufanywa kwa ajili ya Mungu hapa duniani.Mar 175.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents