Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ujumbe wa Msalaba, Sura ya 92

  Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu chochote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu. Wagalatia 6:14.Mar 100.1

  Mungu amenipatia ujumbe kwa ajili ya watu wake... Mmenunuliwa kwa thamani, na jinsi mlivyo na vyote mlivyo navyo vinapaswa kutumika kwa utukufu wa Mungu na kwa faida ya wengine. Kristo alikufa msalabani ili kuokoa ulimwengu toka katika maangamivu ya dhambi. Anaomba ushirikiano wako katika kazi hii. Unapaswa kuwa sehemu ya mkono wake wa kusaidia. Hali ukifanya kwa bidii na juhudi bila kuchoka inapaswa utafute na kuokoa waliopotea. . .Mar 100.2

  Nguvu ya neema ya Kristo inayobadilisha maisha humtengeneza yule ajitoaye kwa huduma ya Mungu. . . Hawezi tena kuendelea katika kutojali roho za wale wanaoangamia karibu naye. . . Anatambua ya kwamba kila sehemu ya uhai wake ni mali ya Kristo, ambaye amemkomboa toka katika utumwa wa dhambi; kwamba kila sehemu ya wakati wake ujao umenunuliwa kwa damu iliyo hai ya thamani ya Mwana pekee wa Mungu.Mar 100.3

  Je, unayo shukrani ya ndani kiasi gani ya kafara iliyotolewa Kalvari? Je, uko tayari kufanya mambo uyapendayo yawe chini ukilinganisha na kazi ya kuokoa roho? Uzito ule ule wa tamaa ya kuokoa wadhambi ambao ulikuwa katika maisha ya Mwokozi unapaswa kusomeka katika maisha ya mfuasi wake wa kweli. Mkristo hana tamaa ya kuishi kwa ajili ya nafsi yake pekee. Ni shauku yake kujitoa yeye mwenyewe na vyote alivyo navyo wakfu kwa ajili ya huduma ya Bwana. Huyu anasisimuliwa na tamaa isiyoelezeka ya kuongoa roho kwa Kristo. . .Mar 100.4

  Je, nawezaje kumtukuza yeye kwa namna iliyo bora zaidi, ambaye mimi ni wake kwa uumbaji na pia kwa ukombozi? Hili ni swali tupaswalo kujiuliza wenyewe. Yeye ambaye ameongoka kweli kweli, atatafuta kwa shauku kubwa kusaidia na kuokoa wale ambao bado wamo chini ya nguvu za Shetani. . . Tunao muda mfupi tu kwa sasa kwa ajili ya kujiandaa na umilele. . . Watu wanahitaji kweli, na kwa uaminifu, kwa bidii tujitahidi kuuwasilisha kwao. Roho zapaswa kutafutwa, zinapaswa kuombewa, zinapaswa kufanyiwa kazi. . .Mar 100.5

  Mabegani mwetu tunao wajibu mzito wa kuuonya ulimwengu juu ya ole unaokuja. . . Mungu analiita kanisa lake liamke na kujivika uwezo. Tunapaswa kuvaa taji zinazodumu; tunapaswa kuupata ufalme wa mbinguni; ulimwengu unaopotea katika kutojua, unapaswa uangaziwe ukweli.Mar 100.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents