Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Imani Isiyoyumba, Sura ya 79

    Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yoyote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Yakobo 1:6Mar 87.1

    Sala na imani lilitenda kazi pamoja, na vinahitajika kujifunzwa pamoja. Katika ombi la imani kuna sayansi ya kimbingu; hii ni sayansi ambayo kila mmoja anayehitaji kuifanya kazi yake iwe na mafanikio anapaswa kuielewa. Kristo anasema, “Yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwawmba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.“ Mk 11:24. Analiweka wazi kwamba kuomba kwetu sharti kupelekane na mapenzi ya Mungu: tunapaswa kuomba mambo aliyotuahidi, na chochote tunachokipokea sharti kitumike katika kutenda mapenzi yake. Masharti yakitimizwa, ahadi yake ni dhahiri.Mar 87.2

    Tunaweza kuomba kwa ajili ya msamaha wa dhambi, kwa ajili ya Roho Mtakatifu, kwa ajili ya kuwa na mwenendo kama wa Kristo, kwa ajili ya hekima na nguvu ya kuifanyia kazi yake, kwa ajili ya karama yoyote ambayo ameahidi: kisha tunapaswa kuamini kuwa tunapokea, na kumshukuru Mungu kwamba tumepokea. Hatuhitaji kutafuta kithibitisho cha baraka. Karama imo katika ile ahadi, na tunaweza kuendelea na kazi zetu tukiwa na uhakika ya kwamba kile alichokiahidi Mungu anao uwezo wa kukitenda, na kwamba ile karama, ambayo tunayo tayari, itatambulika pale tutakapoihitaji hasa.Mar 87.3

    Kuishi namna hiyo kulingana na neno la Mungu maana yake ni kujitoa maisha yote kwake Yeye. Kutakuwa na mwendelezo wa hisia ya kudumu ya uhitaji na utegemezi, hali ya moyo kuvutwa na Mungu. Sala ni hitaji; kwani ni uhai wa roho. Maombi ya kifamilia, maombi ya hadhara, yana mahali pake; lakini ni mahusiano na Mungu yanayodumisha uhai wa roho. . .Mar 87.4

    Kuna mkazo unaoonekana kuliko wakati wowote uliopita ambao unaikamata dunia. Huu mno katika burudani, katika kutafuta pesa, katika kushindania mamlaka, katika kupambana kwa ajili ya maisha, kuna nguvu ya kutisha ambayo inavuta mwili na roho. Kati ya hii hekaheka inayokera, Mungu ananena. Anatuita tukae pembeni na tuwasiliane na Yeye. “Acheni mjue ya kuwa Mimi ni Mungu.”. .Mar 87.5

    Hitaji letu siyo kupumzika kwa muda mfupi tu mbele zake, bali mawasiliano binafsi na Kristo, kuketi katika ushirika na Yeye.Mar 87.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents