Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Hofu Kuu Inayokuja Upesi, Sura ya 130

    Kwa sababu tumekuwa tamasha kwa dunia; kwa malaika na wanadamu. 1 Wakorintho 4:9.Mar 138.1

    Dunia ni ukumbi wa maonesho; wasanii, wakazi wake, wanajiandaa kucheza katika sehemu zao katika igizo la mwisho lililo kuu. Hakuna umoja katika makutano makubwa sana ya watu, isipokuwa pale watu wanapoungana kwa mikataba ili kukamilisha makusudi yao ya kibinafsi. Mungu anatazama. Makusudi yake yahusuyo viumbe wake hawa walio waasi yatatimia. Ulimwengu haujakabidhiwa mikononi mwa watu, hata ingawa Mungu anaruhusu chembe za machafuko na vurugu kutawala kwa muda. Nguvu itokayo chini inatenda kazi ili kuleta taswira kuu za mwisho katika igizo—Shetani ajapo kama Kristo, na atendapo kazi katika wale ambao wamejifunga wenyewe pamoja na jumuiya za siri kwa udanganyifu wote utokanao na kutokuwa na haki. Wale wanaokubaliana na uchu wa mapatano haya wanafanyia kazi mipango ya adui. Utendaji wao huo utakuwa na matokeo.Mar 138.2

    Karibu uasi unafikia kilele chake. Machafuko yanaijaza dunia, na hofu kuu inakaribia kuwafikia wanadamu. Mwisho umekaribia sana. Sisi tuijuao kweli tunapaswa kujiandaa kwa ajili ya kile ambacho kinaujia ulimwengu kama jambo la kushtua sana...Mar 138.3

    Je, tumelala? Laiti vijana wa kike na wa kiume walioko kwenye taasisi zetu ambao sasa hawako tayari kwa ujio wa Bwana, ambao hawajafaa kuwa sehemu ya familia ya Bwana, wangeona ishara za nyakati, tofauti kubwa sana ingeonekana ndani yao! Bwana Yesu anaita watenda kazi walio tayari kujikana nafsi wafuate nyayo zake, watembee na kutendakazi kwa ajili yake, wainue msalaba, na kumfuata pale anapoongoza katika njia.Mar 138.4

    Wengi huridhika kutoa huduma ndogo ndogo kwa Bwana. Ukristo wao ni dhaifu. Kristo alijitoa mwenyewe kwa ajili ya wenye dhambi. Je, tunapaswa kuwa na shauku kiasi gani kwa ajili ya wokovu wa roho tuonapo watu wakiangamia dhambini? Roho hizi zimenunuliwa kwa gharama isiyo kifani. Mauti ya Mwana wa Mungu katika msalaba wa Kalvari ndicho kipimo cha thamani yao. Siku kwa siku wanafanya uamuzi kupata ama uzima wa milele au mauti ya milele.Mar 138.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents