Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mwinue Yesu Kama Kiini, Sura ya 15

    Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi. Ufunuo 22:16.Mar 23.1

    Hatari ya siku ya mwisho inatupa, na katika kazi yetu tunapaswa kuwaonya watu juu ya hatari waliyomo. Matukio nyeti yaliyofunuliwa katika unabii yasije kuachwa bila kusemwa. Watu wetu wangekuwa wameamka kidogo, kama wangejua jinsi matukio yaliyoelezewa katika kitabu cha Ufunuo yalivyokaribia, kungekuwa na uamsho katika makanisa yetu, na watu wengi zaidi wangeuamini ujumbe. Hatuna muda wa kupoteza.... Fundisheni kanuni mpya na mtoe ukweli wa moja kwa moja kwa wingi. Utakuwa kama upanga ukatao kuwili. Lakini msiwe wepesi kuchukua msimamo wa ushindani. Wakati mwingine tutapaswa kutulia na kuuona wokovu wa Mungu. Acheni kitabu cha Danieli kinene, acheni kitabu cha Ufunuo kinene, na kuuelezea ukweli. Lakini, katika hatua yo yote ya ukweli inapotolewa mwinueni Yesu kama kitovu cha matunaini yote, “Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.”Mar 23.2

    Hatuchimbi vya kutosha tunapotafuta ukweli. Kila mtu anayeuamini ukweli wa leo, atafika mahali ambapo atatakiwa kutoa sababu za tumaini lililo ndani yake. Watu wa Mungu watatakiwa kusimama mbele ya wafalme, wakuu, watawala na watu wakuu katika dunia, na wanapaswa kujua kwamba wanaujua ukweli. Wanatakiwa kuwa watu walioongoka. Mungu anaweza kuwafundisha mengi zaidi kwa muda mfupi kuliko mnavyoweza kujifunza kutoka kwa wakuu wa dunia hii. Ulimwengu unaangalia pambano linaloendelea katika dunia. Kwa gharama kubwa”, Mungu ametoa fursa kwa kila mtu kuyajua yale yatakayompatia hekima ili apate wokovu. Malaika wanatazama kwa shauku kubwa kuona ni nani atakayeitumia fursa hii! Ujumbe fulani unapotolewa kwa watu wa Mungu, hawapaswi kuupinga; wanapaswa kuiendea Biblia, wakaupima kwa sheria na ushuhuda, na kama hautapita katika kipimo hicho, utakuwa si wa kweli. Mungu anataka akili zetu zipanuke. Anataka kuiweka neema yake juu yetu. Tunaweza kuwa na karamu ya mambo mema kila siku, kwani Mungu anaweza kutufungulia hazina yote ya mbinguni.Mar 23.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents