Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Hazina Zetu Zote ni kwa Ajili ya Mungu, Sura ya 116

  Mmepata bure, toeni bure. Mathayo 10:8.Mar 124.1

  Vyote ambavyo wanadamu huwa wanapokea kutoka katika fadhila za Mungu, bado ni vya Mungu. Vyote alivyotoa katika vitu vyenye thamani na vizuri vya dunia hii, vimewekwa mikononi mwetu ili kutupima, kupima kina cha upendo wetu kwake na shukurani zetu kwa ajili ya fadhili zake. Kama ni hazina za utajiri au akili, vinapaswa kuwekwa miguuni pa Yesu, kama sadaka za hiari.Mar 124.2

  Alipokuwa akiwatuma wanafunzi wake kwenda “ulimwenguni mwote, mkaihubiri injili kwa kila kiumbe,” Kristo alikabidhi kazi ya kueneza ujuzi wa neema yake kwa wanadamu. Lakini wakati baadhi wanakwenda kuhubiri, anawasihi wengine kutoa sadaka ambazo zitasaidia kazi yake duniani.Mar 124.3

  Si wote wanaoweza kutoa sadaka kubwa, si wote wanaoweza kufanya matendo makuu, matendo ya kusisimua; lakini wote wanaweza kujikana nafsi, wote wanaweza kuonesha tabia ya Mwokozi isiyo na ubinafsi. Baadhi ya watu wanaweza kuleta sadaka kubwa katika hazina ya Bwana; wengine wanaweza kuleta senti chache tu; lakini kila sadaka inayoletwa kwa uaminifu inakubalika na Bwana.Mar 124.4

  Wengi wangeshangaa kuona kiasi ambacho kingepatikana kwa ajili ya kazi ya Mungu kutokana na vitendo vya kujikana nafsi. Pesa kidogo zinazohifadhiwa kutokana na matendo ya kujinyima zitafanya kazi kubwa zaidi ya kuinua kazi ya Mungu kuliko sadaka kubwa zaidi zilizotolewa bila kujinyima. Tabia ya ukarimu ndiyo tabia ya mbinguni. Upendo wa Kristo wa kujitoa mhanga unaonekana pale msalabani. Ili mwanadamu aokolewe, alitoa kila kitu alichokuwa nacho na kisha akajitoa yeye mwenyewe. Msalaba wa Kristo unavuta ukarimu wa kila mfuasi wa Mwokozi aliyebarikiwa. Kanuni aliyoonesha pale msalabani ni kutoa, kutoa. . . Kanuni ya ulimwengu ni kupokea, kupokea. . .Mar 124.5

  Nuru ya injili ikiangaza kutoka katika msalaba wa Kristo inakemea ubinafsi. . . Wengi kati ya watu wa Mungu wako katika hatari ya kunaswa katika mambo ya ulimwengu na tamaa. Inawapasa kuelewa kwamba, rehema yake ndiyo inayoongeza hitaji la mali zao.... Hivyo anamfanya mwanadamu kuwa wenzo wa kugawa baraka zake duniani. Mungu aliweka mpango wa ukarimu ili mwanadamu aweze kufanana na Mwumbaji wake, yaani mkarimu na asiyekuwa na ubanafsi katika tabia yake, na hatimaye apokee ile zawadi tukufu ya milele pamoja na Kristo.Mar 124.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents