Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kupita Malango ya Mbinguni, Sura ya 57

  Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti,...maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu. Waebrania 11:5Mar 65.1

  Tunaishi katika kizazi kiovu. . . Kwa sababu ya kuongezeka kwa maasi, upendo wa wengi unapungua. Henoko alitembea na Mungu kwa miaka mia tatu. Nyakati hizi inaonekana kana kwamba muda kuwa mfupi, ni sababu ya kufanya watu watafute kuwa wenye haki. Je, ni muhimu ya kwamba vitisho vya ile siku ya Mungu viwekwe mbele yetu ili tuhimizwe kutenda yaliyo sahihi? Kisa cha Henoko kinaletwa kwetu. Kwa mamia ya miaka alitembea na Mungu. Hali akiishi katika kizazi potofu; kuchafuka kwa maadili kulipozidi kumzunguka kila mahali; yeye alizoeza akili yake kuabudu, na kupenda usafi. Mjadala wake ulijikita katika mambo ya mbinguni. Aliielimisha akili yake ikimbie katika njia hii, na alidhihirisha uwepo wa mapenzi ya uungu. . .Mar 65.2

  Henoko alikuwa na majaribu kama sisi. Alizingirwa na jamii ambayo haikupatana na haki kama jinsi ilivyo kwetu leo. Hewa aliyovuta ilikuwa imechafuliwa na dhambi na ufisadi, kama ilivyo yetu; na bado aliishi maisha ya utakatifu. Hakuharibiwa na dhambi zilizotawala katika kizazi aIichoish i kwacho. Vivyo hivyo twapaswa kusalia tukiwa safi na bila kupotoshwa. Alikuwa mwakilishi wa watakatifu waishio kati ya hatari kubwa na upotovu katika siku za mwisho. Kwa sababu ya uaminifu wake kwa Mungu alibadilishwa. Vivyo hivyo, wanaosalia kuwa waaminifu, walio hai, watabadilishwa. “Heri wenye moyo safi: maana hao watamwona Mungu.” Kwa miaka mia tatu Henoko alikuwa akitafuta usafi wa moyo, ili awe katika mapatano na mbingu. Kwa karne tatu alikuwa ametembea na Mungu. Siku baada ya siku alitamani ushirika wa karibu zaidi na Mungu; ushirika huu uliendelea kuwaweka karibu zaidi na zaidi, hadi Mungu alipomchukua kwake. Awali alikuwa amesimama katika kingo za ulimwengu unaadumu milele, hatua moja tu kati yake na nchi ya waliobarikiwa; na kisha malango yakafunguka, kule kutembea na Mungu ambako kwa muda mrefu kulishafanyiwa mazoezi hapa duniani, kuliendelea, na akapita katika malango haya na kuingia katika jiji takatifu, akiwa wa kwanza katika wanadamu kuingia pale. . .Mar 65.3

  Mungu anatuita kuingia katika ushirika wa namna hiyo. Kama ilivyokuwa tabia ya utakatifu ya Henoko, ndivyo ipaswavyo kuwa tabia ya wale watakaokombolewa toka kati ya watu wakati wa kuja kwa Bwana mara ya pili.Mar 65.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents