Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kukata Tamaa Kulikofanana, Sura ya 8

    Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma. Yakobo 5:11.Mar 16.1

    Mara nyingi mawazo ya watu, hata walio watumishi wa Mungu, hupofushwa na mawazo ya watu. Mapokeo na mafundisho ya uongo ya watu, husikilizwa kiasi kwamba uelewa wa mambo makuu ambayo Mungu ameyafunua katika Neno lake huwa hafifu. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa wanafunzi wa Kristo, hata wakati Mwokozi alipokuwa nao kimwili. Mawazo yao yalikuwa yamejazwa na dhana iliyopendwa ya matarajio ya kuja kwa Masihi kama mfalme wa muda, ambaye alikuwa aiinue Israeli hadi kufikia katika kiti cha enzi cha kidunia, na hawakuweza kuelewa maana ya maneno yake yaliyotabiri mateso na mauti yake...Mar 16.2

    Tokea kuzaliwa kwao mioyo yao ilikuwa imeelekezwa kwa utukufu uliotegemewa wa ufalme wa kidunia, na hili lilipofusha fahamu zao.Mar 16.3

    Uzoefu wa wanafunzi ambao walihubiri “injili ya ufalme” wakati wa kuja kwake mara ya kwanza, ulipatana na uzoefu wa wale waliotangaza ujumbe wa kuja kwake mara ya pili.Mar 16.4

    Kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wale wa kwanza, William Miller na wenzake hawakuelewa kwa ukamilifu maana ya ujumbe waliokuwa wameubeba. Makosa yaliyokuwa yamedumu kwa muda mrefu kanisani yaliwazuia wasifikie tafsiri sahihi ya jambo muhimu katika unabii. Kwa hiyo, hata ingawa walihubiri ujumbe ambao Mungu alikuwa amewakabidhi ili wautoe kwa dunia, bado kwa sababu ya kutokuelewa maana yake waliingia katika kukata tamaa...Mar 16.5

    Kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa kwanza, kile kilichoonekana kuwa kiza katika fahamu za waumini hawa, kingefanywa kuwa wazi baadaye. Wakati watakapouona “mwisho wa Bwana” watajua ya kwamba, ingawa majaribu yalikuja kutokana na makosa yao, makusudio yake ya upendo kwao yalidumu kutimilika. Wangejifunza kutokana na uzoefu wenye baraka ya kwamba “Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma,” ya kwamba njia zake zote “ni fad hili na kweli kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.”Mar 16.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents