Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kanisa Halitaanguka, Sura ya 24

  Na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda Mathayo 16:18.Mar 32.1

  Wale wanaoshika amri za Mungu na imani ya Yesu watahisi kuinuka kwa Joka pamoja na majeshi yake. Shetani atawachukulia walimwengu kama raia wake, atakuwa ameyadhibiti makanisa yaliyoasi; lakini kutakuwa na kundi dogo litakalokuwa linapinga utawala wake. Kama angeweza kuwafutiliwa mbali katika uso wa dunia, ushindi wake ungekamilika. Kama vile alivyoyaongoza mataifa ya kipagani kuiangamiza Israeli, ndivyo hivi karibuni atakavyozichochea nguvu za uovu duniani kuwaangamiza watu wa Mungu. . . Tumaini lao la pekee litakuwa katika rehema za Mungu; ulinzi wao wa pekee utakuwa maombi. Yohana, akiangalia mbele hadi siku za mwisho, alisema, “Joka alimkasirikia yule mwanamke, akaenda afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu.” Ufu. 12:17. Baadhi ya watu wanaoshi sasa hivi duniani watayaona maneno haya yakitimia.Mar 32.2

  Ghadhabu ya Shetani inaongezeka kadiri muda wake unavyokuwa mfupi, na kazi yake ya udanganyifu na uharibifu itafikia kilele chake katika ule wakati wa tabu.Mar 32.3

  Shetani atafanya miujiza yake ili kudanganya; ataonesha kuwa uwezo wake ni mkubwa kuliko mwingine wo wote. Kanisa litaonekana kana kwamba linaanguka, lakini halitaanguka. Litasimama, wakati wenye dhambi katika Sayuni wakipepetwa—makapi yakitengwa na ngano safi. Hili litakuwa tukio la kutisha sana, lakini ni lazima litukie. Ni wale tu ambao wamekuwa wakishinda kwa damu ya Mwana Kondoo na neno la ushuhuda wake, watakaoonekana watiifu na wakweli, bila doa wala mawaa ya dhambi; bila uongo katika vinywa vyao.Mar 32.4

  Mungu anasema kwamba hata mama anaweza kumsahau mtoto wake, “lakini mimi sitakusahau.”... Mungu anafikiria sana furaha na faraja ya watoto wake na ana kitabu cha kumbukumbu mbele yake, ili asiwasahau watoto wake anaowatunza.Mar 32.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents