Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kwa Nini Mlango wa Rehema Haujwa Fungwa?, Sura ya 84

    Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikilie toba. 2 Petro 3:9.Mar 92.1

    Nilionesliwa hatari yetu kama watu, ya kupatana na ulimwengu zaidi ya sura ya Kristo. Kwa sasa tumo katika kingo za ulimwengu wa milele, lakini ni kusudio la adui wa roho zetu kutuongoza katika kufikiria ya kwamba mwisho wa wakati uko mbali sana. Kwa kila namna iwezayo kufikiriwa, Shetani atawashambulia wale wajiitao kuwa washika amri za Mungu na kudai kuwa wanasubiri kuja kwa mara ya pili kwa Mwokozi atakayekuja na mawingu mbinguni na mamlaka na utukufu mwingi. Atawaongoza wengi kadiri iwezekanavyo kuahirisha siku hii ya hukumu na kuwafanya katika roho zao wawe kama dunia kwa kuiga tabia zake. Nilihisi kutishwa nilipoona ya kwamba roho ya dunia ilitawala mioyo na mawazo ya wengi wanaoukiri ukweli katika hali ya juu....Mar 92.2

    Katika kutafakari juu ya ufupi w a wakati sisi kama watu wake tunapaswa kuwa macho tukisali, kwa namna iwayo yote tusiruhusu mawazo yetu yaondolewe toka kwa kazi iliyo takatifu ya maandalizi kwa ajili ya tukio lile kuu lililo mbele yetu. Kwa sababu wakati unaonekana kuwa umeongezwa, wengi wamekuwa wazembe na wasiojali katika maneno na matendo yao. Hawatambui hatari iliyo mbele yao na hawaelewi rehema za Mungu wetu katika kurefusha muda wa rehema, ili wapate nafasi ya kujenga tabia kwa ajili ya wakati ujao, uzima wa milele. Kila wasaa una thamani kubwa sana. Watu hawapewi muda ili kuutumia katika kujifunza uzembe wao na kuwa wakaaji wa dunia hii, lakini kwa ajili ya kutumika katika kushinda kila udhaifu katika tabia zao na kuwasaidia wengine, kwa kuwa mfano na kwa juhudi binafsi, ili uzuri wa utakatifu wake uonekane. Mungu anao watu duniani ambao kwa imani na tumaini lililo takatifu wanafuatilia kwa karibu sana unabii unaotimia kwa haraka na kutafuta kutakasa roho kwa kuitii kweli, ili wakutwe wakiwa na vazi la harusi Kristo ajapo...Mar 92.3

    Dalili zilizotajwa katika unabii zinatimia kwa kasi kutuzunguka. Hili linapaswa kumsisimua kila mmoja aliye mfuasi wa kweli wa Kristo kutenda kazi kwa moyo.Mar 92.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents