Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ujumbe wa Malaika wa Pili Kurudiwa, Sura ya 163

  “Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanyweshea mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.” Ufunuo 14:8.Mar 171.1

  Ujumbe wa malaika wa pili wa Ufunuo 14 kwa mara ya kwanza uliluibiriwa wakati wa kiangazi mwaka 1844, na kisha ukawa na mvuto mkuu kwa makanisa nchini Marekani, ambapo onyo la hukumu limetangazwa kwa bidii ila likakataliwa na walio wengi, na kasi ya kukataliwa ilikuwa kubwa mno ndani ya makanisa. Lakini ujumbe wa malaika wa pili haukufikia ukamilifu wake hadi mwaka 1844. Hatimaye makanisa yalipitia anguko la kiroho, kama matokeo ya kukataa kwao nuru ya ujumbe wa Marejeo ya Kristo; ila anguko hilo lilikuwa halijakamiIika bado. Kadiri walivyoendelea kuukataa ukweli maalumu kwa kizazi hiki walizidi kudidimia kiroho. Hata hivyo hadi sasa haiwezi kusemwa, “Babeli imeanguka, . . . maana ndio uliowanyweshea mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.” Bado hajayanywesha mataifa yote mvinyo huu.Mar 171.2

  Mungu bado anao watu katika Babeli; na kabla ya kumwagwa kwa ghadhabu yake watakatifu hao sharti waitwe wapate kutoka, wasishiriki dhambi zake na “wasipokee mapigo yake.”Mar 171.3

  Huu ni ujumbe ule ule uliotolewa na malaika wa pili. Babeli umeanguka, “maana ndio uliowanyweshea mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.” Je mvinyo ni nini?—ni mafundisho yake ya uongo. Ameupatia ulimwengu sabato ya uongo badala ya Sabato ya amri ya nne, naye amerudia uongo ambao Shetani hapo mwanzoni alimwatnbia Hawa pale Edeni —kwamba roho kwa asili haifi. Mafundisho tele ya uongo wa aina hiyo ameyasambaza mbali na pote “akiyafundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu”. . .Mar 171.4

  Katika kazi ya mwisho ya kuuonya ulimwengu, wito wa aina mbili maalumu umetolewa kwa makanisa. Ujumbe wa malaika wa pili ni, “Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.” Na katika kilio kikuu cha ujumbe wa malaika wa tatu sauti ilisikika kutoka mbinguni ikisema, “Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.”Mar 171.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents