Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Vitu vya Bandia, Sura ya 148

    “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, hila shaka kwa hao hapana asubuhi.” Isaya 8:20Mar 156.1

    Watu wa Mungu wameelekezwa kwenye Maandiko kama kinga yao dhidi ya ushawishi wa walimu wa uongo na uwezo wa kudanganya wa pepo wa giza. Shetani anatumia kila mbinu inayowezekana ili kwamba watu wasipate maarifa ya Biblia; kwani maelezo ya wazi ya Biblia yanatumia udanganyifu wake. Kwa kila uamsho wa kazi ya Mungu, mfalme wa giza anaamka ili kushughulika kwa bidii zaidi; na sasa anaongeza juhudi zake kwa kiwango cha juu kabisa kwa ajili ya pambano la mwisho kati yake na Kristo pamoja na wafuasi wake. Udanganyifu mkuu wa mwisho karibuni utatokea mbele yetu. Mpinga Kristo atatenda kazi zake za ajabu mbele ya macho yetu. Maajabu hayo ya bandia yatafanana sana na miujiza ya kweli kiasi kwamba itakuwa ni vigumu kuyapambanua isipokuwa kwa njia ya Maandiko Matakatifu. Kila kauli na kila muujiza ni lazima vijaribiwe kwa ushuhuda wake.Mar 156.2

    Mtu anayefanya utendaji wa miujiza kuwa ndio kipimo cha imani yake, atagundua kuwa kupitia udanganyifu wa aina mbalimbali, Shetani anaweza kufanya maajabu ambayo yataonekana kama miujiza ya kweli.Mar 156.3

    Shetani anatenda kwa hila sana, naye ataingiza imani potofu kanisani ili kuchanganya na kupofusha akili za watu na kuondolea mbali mafundisho ya wokovu. Wale ambao hawalipokei Neno la Mungu kama linavyosomeka, watanaswa katika mtego wake.Mar 156.4

    Malaika waovu wamo njiani mwetu kila wakati. ... watajitwalia maeneo mapya na kutenda maajabu na miujiza mbele ya macho yetu.Mar 156.5

    Wengine watajaribiwa kupokea maajabu kama yanayotoka kwa Mungu, wagonjwa wataponywa mbele yetu. Miujiza itafanyika mbele ya macho yetu. Je, tumejiandaa kwa ajili ya jaribu linalotungojea wakati maajabu ya uongo ya Shetani yatakapodhihirishwa kikamilifu? Je, roho nyingi hazitanaswa na kuchukuliwa? Kwa kuacha maagizo na amri za Mungu, na kusikiliza hadithi za uongo, akili za watu wengi zinajiandaa kupokea maajabu hayo ya uongo. Sote tunapaswa kuvaa silaha sasa kwa ajili ya pambano ambalo tutakabiliana nalo hivi karibuni. Imani katika Neno la Mungu, ambalo kama tukiIisoma kwa maombi na kulitendea kazi maishani, Litakuwa ndiyo ngao yetu dhidi ya nguvu za Shetani na litatufanya kuwa washindi kwa damu ya Kristo.Mar 156.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents