Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Upinzani na Mateso, Sura ya 23

    Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu, watalishika na lenu. Yohana 15:20.Mar 31.1

    Mateso katika namna zake zote ni kuinuka kwa kanuni ambayo itaendelea kuwapo ili mradi Shetani yupo na Ukristo una nguvu yake nyeti. Hakuna mtu anayeweza kumtumikia Mungu bila kujisababishia upinzani kutoka katika majeshi ya giza. Malaika waovu watamshambulia, wakiona kwamba ushawishi wake unawanyang’anya mawindo yao. Watu waovu, waliokemewa na mfano wa maisha yake, wataungana na malaika hao wakitaka kumfarakanisha na Mungu kwa majaribu yenye ushawishi mkubwa. Mambo haya yasipofanikiwa, basi nguvu ya kushurutisha Hutumika kuilazimisha dhamira yake.Mar 31.2

    Lakini kadiri Yesu anavyoendelea kuwa mwombezi wa wanadamu katika hekalu la mbunguni, udhibiti wa Roho Mtakatifu utawagusa watawala pamoja na watu. Kwa kiasi fulani bado unadhibiti sheria za nchi. Kama isingekuwa sheria hizi, hali ya ulimwengu ingekuwa mbaya kuliko ilivyo sasa. Wakati wengi kati ya watawala wetu ni mawakala wa Shetani; Mungu pia ana mawakala wake miongoni mwa viongozi wa mataifa. Adui anawaongoza watumishi wake kupendekeza hatua ambazo zingeathiri sana kazi ya Mungu; lakini viongozi wanaomcha Bwana wakiongozwa na malaika watakatifu watapinga mapendekezo hayo kwa hoja zisizopingika. Kwa njia hiyo watu wachache watadhibiti wimbi kali la uovu. Upinzani wa wale maadui wa ukweli utadhibitiwa ili ujumbe wa malaika wa tatu ufanye kazi yake. Onyo la mwisho likisha kutolewa, Iitavuta usikivu wa viongozi hawa ambao Bwana anawatumia kwa sasa, na baadhi yao watalipokea, nao watasimama pamoja na watu wa Mungu katika wakati wa taabu. . .Mar 31.3

    “Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu. . .” Yoe. 2:23. “Itakuwa katika siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu.” “Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.” Mdo. 2:17, 21.Mar 31.4

    Kazi kubwa ya Injili haitafungwa kwa udhihirisho mdogo wa Uwezo wa Mungu kuliko ule ulikuwepo wakati ilipoanza.Mar 31.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents