Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kupotoa Maandiko, Sura ya 124

  Na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara,... huyapotoa,... maandiko, kwa uvunjifu wao wenyewe. 2 Petro 3:16.Mar 132.1

  Mojawapo ya udanganyifu wa Shetani ambao umefanikiwa zaidi ni ule wa imani ya kwamba hakuna sababu ya kujali imani walizonazo watu. Shetani anajua ya kuwa ukweli, ukipokelewa kwa kupendwa, utatakasa roho ya mpokeaji; kwa hiyo anajitahidi bila kukoma kutafuta namna ya kuweka nadharia, hadithi na injili za uongo badala ya ukweli. . .Mar 132.2

  Fafanuzi zitokanazo na ubunifu na zenye mashaka za Maandiko, na nadharia nyingi zinazopingana kuhusu imani ya kidini, ambazo zinapatikana katika ulimwengu wa Kikristo ni kazi ya adui yetu mkuu inayokusudia kutchanganya mawazo ili yasiweze kuuona ukweli. Kwa kiasi kikubwa kutokuelewana na mgawanyiko uliopo kati ya makanisa ya Kikristo kunatokana na desturi ya kupotoa Maandiko ili kuunga mkono nadharia inayopendwa. Wengi wanatafuta kugundua kitu fulani kigeni au kuwa wa kwanza kusema dhana fulani, badala ya kujifunza kwa uangalifu neno la Mungu kwa unyenyekevu wa moyo ili kupata ujuzi wa mapenzi yake.Mar 132.3

  Kwa makusudi ya kuendeleza mafundisho yasiyo sahihi au mazoea yasiyo ya Kikristo, wapo ambao hukamata sehemu fulani za Maandiko ambazo zimenukuliwa bila kuzingatia muktadha, pengine kwa kunukuu nusu ya fungu kwa makusudi ya kuthibitisha kauli zao, wakati ambapo sehemu inayosalia ya fungu ingeonesha maana ambayo ni tofauti kabisa. Kwa kufuata hila za Joka wanajichimbia handaki wenyewe nyuma ya kauli zisizo na muunganiko ambazo zimefumwa ili zipatane na tamaa za mwili. Kwa namna hiyo, wengi Wanapotosha kwa makusudi neno la Mungu. Wengine ambao wana uwezo zaidi wa kufikiri, huwa wanakamata vielelezo na mifano iliyo katika Maandiko Matakatifu, na kuyafasiri kulingana na ubunifu wao, huku wakikosa heshima kwa ushuhuda wa Maandiko kama yawezayo kujifasiri yenyewe, kisha wanawasilisha mawazo yao yasiyo ya kawaida kama ndiyo mafundisho ya Biblia.Mar 132.4

  Wakati wowote Maandiko yanaposomwa bila roho yenye sala, unyenyekevu, na inayofundishika, aya zilizo wazi kabisa na rahisi na zile zilizo ngumu zitapotoshwa kutoka katika maana yake halisi. . . Neno la Mungu liko wazi kwa wote wanaolisoma wakiwa na mioyo iliyojaa sala. Kila roho ya kweli na aminifu itakutana na nuru ya kweli. “Nuru imemzukia mwenye haki.” Zab. 97:11. Hakuna kanisa liwezalo kukua katika utakatifu kama washiriki wake hawaitafuti kweli kwa dhati kama watafutao hazina iliyofichwa.Mar 132.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents