Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wakati wa Kupimwa, Sura ya 34

    Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa Maarifa, na matendo hupimwa na yeye kwa mizani. 1 Samweli 2:3Mar 42.1

    Nimeona malaika amesimama akiwa na mizani mikononi mwake, akiyapima mawazo na matakwa ya watu wa Mungu, na hasa vijana. Upande mmoja wa mizani kulikuwa na mawazo na matakwa yanayowaelekeza mbinguni; upande mwingine kulikuwa na mawazo na matakwa yanayowaelekeza duniani. Na upande huu kuliwekwa vitabu vyote vya hadithi, mawazo ya mavazi na kujionesha, ubatili, kiburi, na kadhalika. Ni wakati nyeti sana! Malaika wa Mungu wakiwa na mizani wanapima mawazo ya wale wanaodai kuwa watoto wake—wale wanaodai kuwa wameufia ulimwengu na kuishi kwa ajili ya Mungu. Upande uliojaa mawazo ya duniani, ubatili, na kiburi ulishuka chini upesi, pamoja na kwamba vingi vilikuwa vinamwagika kutoka upande huo. Upande uliokuwa na mawazo ya mbinguni uli panda juu upesi wakati ule mwingine ukishuka chini, na ulikuwa mwepesi sana. Ninaweza kusimulia jambo hili kama nilivyoliona; lakini siwezi kuonesha mguso bayana na wa pekee ulioaehwa katika akili yangu, wakati nikimwona yule malaika akipima mawazo na matakwa ya watu wa Mungu. Kisha malaika akasema: “Je, hawa wanaweza kuingia mbinguni? Hapana, hapana, haiwezekani. Waambie kuwa matumaini waliyo nayo sasa hivi ni ya bure, na wasipotubu haraka na kupokea wokovu, wataangamia.”. . .Mar 42.2

    Niliona kwamba wengi walikuwa wanajipima wao kwa wao, na kuyalinganisha maisha yao na ya wengine. Haipasi kuwa hivyo. Hatujapewa mtu mwingine zaidi ya Kristo kuwa mfano wetu. Yeye ni mfano wetu wa kweli, na kila mmoja anapaswa kujitahidi kumwiga kwa ufanisi. . . .Mar 42.3

    Niliona kuwa wengi hawajui bado maana ya kujikana au kujitoa mhanga, au maana ya kuteseka kwa ajili ya ukweli. Lakini hakuna atakayeingia mbinguni bila kujitoa mhanga. Lazima moyo wa kujikana na kujitoa mhanga ukuzwe. Baadhi hawajajitoa mhanga, yaani kutoa miili yao katika madhabahu ya Mungu. Wanaendekeza hasira ya haraka, wanaendekeza uchu, na wanashughulikia matakwa yao wenyewe, bila kujali kazi ya Mungu. Wale walio tayari kujinyima kwa namna yo yote ile kwa ajili ya uzima wa milele, wataupata: na itakuwa faida kubwa hata kama ni kuteseka ili kuupata, uthamani wake unastahili kuisulubisha nafsi ili kuupata, na pia kutoa sanamu zote ili kuupata. Utukufu mkubwa usio wa kawaida na ulio mzito kabisa utameza na kufunika kila anasa ya kidunia.Mar 42.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents